Connect with us

General News

Marais Kenyatta na Magufuli wapigia debe ushirikishi wa wafanyibiashara wadogo

Published

on

Loading...

[ad_1]

Marais Uhuru Kenyatta na John Pombe Magufuli wa Tanzania  leo walipigia debe ufanikishaji wa wafanyibiashara ndogo-ndogo walipozindua kituo cha pamoja cha mpakani cha Namanga (OSBP).

Wakizungumza baada ya kuzindua kituo hicho huko Namanga, Rais Kenyatta na Rais Magufuli walisema kituo hicho cha mpakani kinaashiria mwanzo mpya wa ushirikiano utakaohakikisha kunawiri kwa biashara na kunufaika vilivyo kwa wenye biashara ndogo-ndogo.

Rais Kenyatta alitahadharisha maafisa wa forodha na uhamiaji wa mataifa haya mawili katika kituo hicho cha mpakani dhidi ya kujihusisha na ufisadi akisema uovu huo unahujumu azima ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyolenga uchukuzi wa watu na bidha.

“Tumetambua kwamba mara nyingi biashara kati ya mataifa haya mawili huvurugwa na maafisa waliopewa majukumu ya kusimamia vituo vyetu vya mipakani. Badala ya maafisa hawa kuwasaidia raia kufanya biashara kwa njia huru wanajihusisha na ufisadi. Sharti haya yakome,” kasema Rais Kenyatta.

uhuurandmagufuliatborder
Uhuru Kenyatta and John Magufuli

Rais alisistiza kwamba sababu ya kuweka kituo cha pamoja mpakani ni kuimarisha uwezo wa wafanyibiashara kutoka mataifa haya mawili kuendesha biashara zao.

‘He said I was looking for people to rape me’, Kenyan open transgender Letoya Johnstone narrates

Alisema kwamba  ni wenye biashara ndogo-ndogo wanaochangia sana ukuaji wa uchumi wa Kenya, hivyo basi wanastahili kuungwa mkono kufanya biashara kwenye pande zote za mpaka bila vikwazo vyovyote.

 “Ndio maana nakubaliana na Rais Magufuli kwamba tukiwa viongozi ni wajibu wetu tunapoendelea kuimarisha biashara kati ya mataifa haya mawili, sharti tuhakikishe kwamba tunawalinda wenye biashara ndogo-ndogo. Hilo ndilo tunalolitaka ili kila raia wa Jumuiya ya Afrika Mashariki aweze kunufaika,” kasema Rais Kenyatta.

Hata hivyo, Rais Kenyatta alisema wafanyibiashara wa Mataifa haya mawili hawapaswi kutumia vibaya nafasi wanazopewa katika kituo hicho cha mpakani kwa kushirki biashara haramu.

uhuruanfmagufulichat
Kenyan President Kenyatta and Tanzanian President Magufuli

Rais Kenyatta alisema anaridhishwa na  tangazo la Benki ya Maendeleo Barani Afrika kwamba itafadhili ujenzi wa barabara kuu ya Malindi kupitia Lunga Lunga nchini  Kenya hadi Bagamoyo nchini Tanzania, akisema barabara hiyo itaboresha juhudi za mshikamano wa kanda hii kwa kiwango kikubwa.

Akisistiza umuhimu wa mshikamano, Rais Kenyatta alikariri wito wake kwa raia wa Afrika Mashariki kutoruhusu mipaka iliyobuniwa na wakoloni kuwagawanya.

“Mipaka hii iliyobuniwa na wakoloni haistahili kugawanya jamii ambazo zimeishi pamoja na kushirkiana kwa miaka mingi,” kasema Rais.

Loading...

Alisema kanda hii inastahili kulenga kushirikisha mataifa sita ya Jumiya ya Afrika Mashariki kuboresha soko la pamoja lenye idadi ya watu milioni 200 akisema hatua hiyo itawezesha eneo la Afrika Mashariki kuendesha biashara kikamilifu na mashirikisho mengine ya kiuchumi ndani na nje ya bara la Afrika.

“Ushirikishi wetu na soko la pamoja utavutia waekezaji zaidi na kubuni nafasi za kazi kwa watu wetu,” kasema Rais Kenyatta.

uhurugreetsmagufuli
Uhuru Kenyatta and John Magufuli at the Namanga Border

Kituo cha pamoja cha Namanga ni kimoja kati ya vituo 15 kama hicho katika kanda jii na cha kwanza kilichozinduliwa ni cha Taveta-Holili kilichoanzishwa Mwezi Februari mwaka 2016.

Rais Magufuli alisema kituo cha pamoja cha Namanga kitarahisisha biashara na kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Kenya na Tanzania.

Rais Magufuli alisema vituo vya pamoja mipakani vimeleta mafanikio mengi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki akitoa mfano wa kupungua kwa gharama ya uchukuzi, kupunguzwa kwa muda wa usafiri, kuongezeka kwa biashara pamoja na utalii.

“Inatarajiwa kuwa kituo hicho cha pamoja mpakani kitafanikisha na kuimarisha biashara. Wafanyibiashara wataweza kusafirisha bidhaa zao kwa wakati mara 10 kwa mwezi ilihali nyakati zilizopita ilikuwa vigumu kufanya hivyo hata mara nne kwa mwezi,” kasema Rais Magufuli.

Alisema kituo hicho cha pamoja mpakani kimeongeza pia ukushanyaji ushuru kutoka shilingi bilioni 3 hadi shilingi bilioni 4.5 za Tanzania kila mwezi tangu kianze shughuli mwezi Oktoba mwaka jana.

Rais Magufuli alisema kuwa kimoja kati ya vitu vinavyotatiza ushirikiano wa kiuchumi miongoni mwa mataifa barani Afrika ni changamoto ya ushirikishi wa biashara kutokana na kucheleshwa bila sababu   kwa mizigo barabarani, bandarini na katika vituo vya mapakani na hivyo kuongeza gharama ya kufanya biashara.

Also read more here

“Kulingana na utafiti wa Benki ya Dunia changamoto kama hizo husababisha aslimia 65 ya gharama ya kufanya biashara barani Afrika. Hali hii husababisha gharama ya juu ya kuendesha biashara barani Afrika ikilinganishwa na mataifa mengine. Kwa mfano  inakisiwa kwamba gharama ya kufanya biashara Amerika kusini ni mara tatu juu zaidi na mara tano zaidi  katika bara Asia,” kasema Kiongozi wa Taifa la Tanzania.

Alisema gharama kubwa ya kufanya biashara pia hupunguza husababisha kupungua kwa biashara kati ya mataifa ya bara la Afrika ikilinganishwa na bara nyingine na kwamba hatua hiyo huchangia katika kuvutia waekezaji wachache wa kigeni.

Wengine waliozungumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na Mawaziri Peter Munya, James Macharia, Keriako Tobiko na Adan Mohamed ni Gavana wa Kajiado Joseph Ole Lenku, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Balozi Liberat Mufumukeko na Balozi wa Japan nchini Tanzania Shinichi Goto miongoni mwa wengine.[ad_2]

Source link

Loading...
Advertisement
Loading...
Loading...

Facebook

Loading...

Trending