Connect with us

General News

12 wafariki kwenye ajali Naivasha – Taifa Leo

Published

on

12 wafariki kwenye ajali Naivasha – Taifa Leo


12 wafariki kwenye ajali Naivasha

NA MACHARIA MWANGI

WATU si chini ya 12 wamethibitishwa kufariki baada ya basi la Chuo Kikuu cha Pwani kugonga matatu katika eneo la Kayole kwenye barabara ya Naivasha-Nakuru.

Naibu kamishna Kisilu Mutua amethibitisha na kuongeza huenda miili zaidi ikaondolewa kwenye basi.

“Hii ndiyo idadi ya hivi punde lakini ninaendelea kupata habari zaidi kutoka kwa maafisa wa polisi na vitengo mbalimbali vya hospitali zilizoko katika eneo hili,” amesema afisa huyo wa utawala.

Magari hayo mawili – basi na matatu husika –  yalikuwa yakielekea upande wa Nakuru.

Mwanamke aliyeshuhudia ajali hiyo, Bi Ruth Wambui, amesema basi limepoteza mwelekeo baada ya kugonga matatu iliyokuwa ikiingia kwa barabara kuu baada ya kuchukua abiria kando ya barabara.

“Dereva wa basi amepiga honi mara kadhaa huku likaribia kwa kasi ya juu,” amesema Bi Wambui.

Naye Simon Njoroge ambaye pia ameshuhudia amesema breki za basi zimekataa kufanya kazi kwenye mteremko.

“Basi limegonga matatu mara mbili kabla ya kuingia kwenye mtaro kando ya barabara,” amesema Bw Njoroge.

Ajali hutokea mara kwa mara kwenye maeneo yaliyoko katika barabara ya Naivasha-Nakuru.Source link

Comments

comments

Facebook

Trending