Connect with us

General News

AFCON 2019: Mshambulizi wa Tunisia Wahbi Khazri matatani baada ya kumtandika kocha wa Senegal ▷ Kenya News

Published

on


Mshambuzi wa Tunisia Wahbi Khazri, huenda akapigwa marufu kushiriki mechi za kimataifa baada ya kudaiwa kumpiga kocha wa Senegal Aliou Cissé baada ya mechi ya nusu-fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) iliyosakatwa mnamo Jumapili.

Bao la kujifunga la Dylan Bronn wakati wa muda wa ziada liliisaidia Senegal kufuzu kuingia katika fainali na kuvaana tena na Algeria ambao walizamisha Nigeria katika mechi ingine ya nusu-fainali.

Habari Nyingine: Senegal vs Tunisia: Goli la kujifunga la Dylan Bronn lawapa Simba wa Teranga ushindi

Habari Nyingine: Algeria vs Nigeria: Mkwaju wa adhabu wa Riyad Mahrez wavunja Wanigeria nyoyo

Mechi kati ya Senegal na Tunisia ilikumbwa na vitimbi aina yake huku timu zote mbili zikipigania nafasi ya kuingia kwenye fainali ya mshindano hayo.

Mechi hiyo ililazimika kuingia katika muda wa ziada baada ya kumaliza droo tasa katika muda wa kawaida, huku timu zote zikikosa kuonja wavu licha ya kuwa na nafasi nzuri kufunga mabao zikiwemo penalti mbili katika upande zote mbili

Hata hivyo, penalti ya kutiliwa shaka ya Tunisia iliyoamuliwa na video ya VAR, ilikuwa kilele cha mechi hiyo huku wachezajai wakinaswa kwenye kamera waking’ang’ania kuingia kwenye fainali.

Habari Nyingine: AFCON 2019: Mafundi wa utingaji mabao Afrika

Ripoti kutoka kwa vyombo vya habari vinaripoti kuwa Khazri, ambaye ni nahodha msaidizi wa Carthage Eagles, aliingia katika upande wa ushauri wa Senegal na kumpiga Cisse ambaye ni kocha wa sasa wa timu hiyo.

Bado haijabainika wazi nini kilichomkasirisha kijana huyo wa Saint-Étienne ambaye kwa sasa kuna uwezekano wa kumpiga marufuku kushiriki mchezo huo.

READ ENGLISH VERSION

Taarifa yake Kevin Kimutai, mwandishi wa TUKO.co.ke

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko News

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending