Connect with us

General News

Algeria vs Nigeria: Mpira wa adhabu wa Riyad Mahrez wavunja Wanigeria nyoyo ▷ Kenya News

Published

on


Algeria wamefuzu kwa fainali ya kombe la taifa bingwa barani Afrika makala ya 2019 baada ya kuwatandika Super Eagles wa Nigeria mabao 2 -1 mnamo Jumapili Julai 14 katika uwanja wa Cairo International Stadium.

Mbweha wa Jangwani kutoka Algeria walianza mechi kwa mbwembwe katika kipindi cha kwanza na nusura wafunge goli la kwanza katika dakika ya 8 lakini golikipa wa Nigeria Daniel Akpeyi alikuwa imara na kuchangamkia hatari kubwa.

Habari Nyingine: AFCON 2019: Algeria yapepeta Ivory Coast 4-3 kufuzu nusu-fainali

Habari Nyingine: AFCON 2019: Mafundi wa utingaji mabao Afrika

Difenda wa Super Eagles Kenneth Omeruo alishindwa kuondosha pasi ambayo nusura iipe Algeria goli ya ufunguzi lakini Mohamed Belaili alishindwa kuitumia fursa hiyo.

Hata hivyo, Algeria ilifunga bao la kwanza muda mfupi kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza baada ya difenda wa Nigeria William Troost- Ekong kufunga katika lango lake mnamo dakika ya 40.

Habari Nyingine: Tanzania yamteua kocha mpya wa timu ya Taifa Stars

Nigeria ilisawazisha mambo katika dakika ya 73 baada ya Aissa Mandi kunawa mpira katika eneo la penalti ambapo refa aliipa Nigeria penalti baada ya kuangalia video ya kumsaidia refa kufuatia matukio ya mechi.

Mshambulizi wa Nigeria Odion Ighalo aliifungia Nigeria goli la nne la kinyang’anyiro hicho.

Lakini nyoyo za WaNigeria zilivujwa kunako dakika za lala salama pale mshambulizi wa Manchester City Riyad Mahrez alipofunga kwa ufundi mkubwa kutokana na mpira wa adhabu, na hivyo kuipa Algeria ushindi wa 2 -1.

Algeria sasa itaonana kijasho na Senegal katika fainali ya kombe la taifa bingwa barani Afrika.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending