Connect with us

General News

Aliyekuwa Waziri wa Michezo Rashid Echesa aanza kumkwepa DP William Ruto ▷ Kenya News

Published

on


– Echesa amesema hatamuunga mkono Ruto bila yeye kuwapa Waluhya mgao mkubwa kwenye serikali yake

– Mwanasiasa huyo alisema Raila aliwasahau wafuasi wake na kujiunga na Uhuru

– Waziri huyo wa zamani alisema sasa siasa zake zitakuwa za kuinufaisha jamii yake

Aliyekuwa Waziri wa Michezo Rashid Echesa anaonekana anaendelea kumkwepa Naibu Rais William Ruto tangu alipochujwa kutoka kwenye baraza la mawaziri.

Akiongea Jumatatu, Julai 15, Echesa alisema atamuunga mkono Ruto iwapo tu ataelezea manufaa watakayopata watu kutoka jamii ya Waluhya ndani ya serikali yake.

Habari Nyingine: Katibu mkuu wa Jubilee Raphael Tuju apuuza madai ya Ruto, kuendelea kumshauri Raila

Rais Uhuru Kenyatta, Raila Odinga na Rashid Echesa. Picha: Nation
Source: UGC

Vile vile, mwanasiasa huyo alisema kuwa eneo la magharibi haliwezi kumuunga mkono tena kiongozi wa ODM Raila Odinga kwani amekosa kufaulu urais mara mingi.

-Echesa”Tumechoka na kucheza na maisha ya watu wetu, tumekuwa tukimuunga mkono mara mingi bila ya matunda yoyote. Aliwaambia anawapeleka Canaan lakini akajiunga na washindani wake baadaye,” Echesa alisema.

Habari Nyingine: Mwizi aandika barua ya kuomba msamaha baada ya kukosa sadaka kanisani

Aliyekuwa Waziri wa Michezo Rashid Echesa aanza kumkwepa DP William Ruto

Aliyekuwa Waziri wa Michezo Rashid Echesa. Picha: TUKO.co.ke
Source: Original

Hapo awali, waziri huyo wa zamani alikuwa ni mfuasi mkuu wa chama cha Jubilee na Naibu Rais William Ruto huku akimpigia debe pakubwa.

Hilo kwa sasa linaonekana kuwa yaliyopita kwani anaweka masharti ya kumpigia Ruto debe.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending