Connect with us

General News

Baraza la Sanaa Tanzania lamfungia mwanamuziki Rosa Ree miezi 6, haruhusiwi kufanya muziki ▷ Kenya News

Published

on


Baraza la Sanaa nchini Tanzania, BASATA limemfungia miezi 6 msanii nyota wa muziki wa hip hop hapa Rosa Ree kutojihusisha na shughuli zozote za kimuziki

Hii ni kufuatia wimbo wake mpya wa ‘Vitamin U’ ambao ulikashifiwa vikali kote Tanzania na humu nchini kwa kuwa mchafu.

Habari Nyingine: Mchungaji akasirishwa na makapera wa kanisa lake

Rosa Ree alikuwa amemshirikisha mwanamuziki Timmy Tdat wa hapa Kenya ambaye inasemekana ni mpenzi wake.

Habari Nyingine: Migori: Jombi atandikwa na wake zake kupanga kuoa mke wa tatu

Hata hivyo, baraza hilo halikuelezea iwapo mwanamuziki huyo amepigwa marufuku ya kushiriki shughuli za muziki nchini humo pekee au hata katika nchi za nje.

Kulingana na baraza hilo, Rosa Ree alikashifiwa kwa makosa matatu likiwemo la kuachia video inayokiuka maadili ya kitanzania na kumshirikisha mwanamuziki wa nchi ya nje bila kibali kutoka katika baraza hilo.

Habari Nyingine: Sarah Cohen aomba mahakama aruhusiwe kufika kwake kuchukua mvinyo

Rosa Ree tayari amepigwa faini ya TSh 2 milioni kwa makosa hayo.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending