Connect with us

General News

Embu: Jamaa azimia kupata mke amehepa na ATM ▷ Kenya News

Published

on


Wakazi wa Kyeni, jimbo la Embu walishuhudia sinema ya bure kwenye ploti moja baada ya mwanaume kuzimia alipogundua mkewe ametoweka na kadi yake ya ATM.

Mzozo ulizuka pale ambapo mke alianza kumshutumu mumewe kwa kutumia pesa zake kuwafurahisha vipusa wengine nje ya ndoa.

Habari Nyingine: Kalameni azua sarakasi kwa mama pima mvinyo ulipokolea

Penyenye zinaarifu kwamba, wawili hao walioana wakiwa maskini lakini baada ya kufunga ndoa maisha yao yaliimarika biashara zao ziliponawiri.

Kwa mujibu wa Taifa Leo, jamaa alijiona bwenyenye na akaanza kufukuzana na warembo wa chuo kikuu, tabia ambayo ilimkera mkewe.

Habari Nyingine: Mwanamuziki Sanaipei Tande awavalia ‘team mafisi’ bikini, awaacha taabani

Mkewe alipoona jamaa harekebishi tabia wala hata kumsikiza, alipanga kuondoka bila kuaga kwa heri huku akiapa kumfunza jamaa adabu ya mwaka.

Inaarifiwa kwamba mke alifanikiwa kumshawishi jamaa wachukue mkopo wa KSh 1 milioni ili wanunue ploti.

Siku moja wakati jamaa alikuwa hayupo nyumbani, mwanadada aliwahi ATM na kuondoka.

Duru zinafichua kwamba baada ya jamaa kuarifiwa kwamba mkewe alionekana akiondoka, aliwasili chumbani mwao kubaini ukweli wa mambo na hapo ndipo alipozimia kugundua ATM haipo na mke ameondoka na bidhaa zingine za thamani.

Habari Nyingine: Zari Hassan kuhama kwenye nyumba ya Diamond ilioko Afrika Kusini

Jamaa alikemewa na majirani waliofika kumpa huduma ya kwanza wakimwarifu kwamba alistahili yaliyomfika kwa kumdharau mkewe licha ya bidii yake kuboresha maisha yao.

“Hilo litakuwa funzo kwako na wanaume wote mtaani wanaojifanya viherehere baada ya kupata pesa. Kama mlianza maisha ya dhiki na mke wako mbona huendelei kunyenyekea hata baada ya kufanikiwa? Pambana na hali yako sasa, sisi tulifika kuokoa maisha yako,” majirani walisuta.

Penyenye zinaarifu kwamba jamaa alijifungia chumbani mwake siku mbili baada ya kuandamwa na mawazo.

Habari Nyingine: Mama mzazi wa Peter Kenneth Rahab Wambui ameaga dunia

Inasemekana jombi alishindwa pa kuanzia kwani hangemchukulia hatua yoyote mkewe kwani akaunti ilikuwa yao wawili na pia ni yeye aliyempa nambari ya siri ATM.

Juhudi zake za kumsaka mkewe zilitumbukia nyongo kwani mwanadada alikatiza mawasiliano naye ila alikuwa akizungumza na marafiki za jamaa tu.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending