Connect with us

General News

Ezra Chiloba sasa anataka kulipwa fidia ya KSh 52.5 milioni kutoka kwa IEBC ▷ Kenya News

Published

on

Loading...


Mwaka mmoja sasa tangia kufurushwa kwake ofisini, katika jumba la Anniversary Towers, aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Ezra Chiloba, amefika kortini akitakata kulipwa fidia.

Chiloba, kupitia kwa kesi iliyowasilishwa na kampuni ya mawakili ya Wandabwa, anataka kulipwa fidia ya KSh 52.5 milioni kwa kufutwa kazi kwa njia isiyokuwa halali.

Habari Nyingine: Wakenya wahisi Cohen alikuwa sawa kumfungia Sarah nje kwenye urathi wake

Chiloba

Alikuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa IEBC Ezra Chiloba.
Source: UGC

Habari Nyingine: Kakamega: Familia yaishi kwa hofu baada ya radi kupiga na kupasua mti bomani mwao

Kesi hiyo iliyowasilishwa kwa mahakama ya Leba, mlalamishi anadai kuwa njia iliyotumiwa na maafisa wa kuu wa tume hiyo haikuwa halali na pia Chiloba hakupewa nafasi ya kujitetea, kama ilivyoripoti gazeti la Daily Nation ya Jumapili, Septemba 22.

“Madai ya mlalamishi yanakujia kutokana na hatua ya 1EBC ambayo ilikuwa kinyume cha sheria, njia isiyokubalika na pia sio halali ambayo inaweza kulinganishwa na 1. Mapumziko ya lazima 2. kupigwa marufuku na 3. kutamatishwa kwa mkataba wake,” ilisoma taarifa hiyo kutoka kwa mlalamishi.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Loading...

Source link

Comments

comments

Loading...
Advertisement
Loading...
Loading...

Facebook

Loading...

Trending