Connect with us

General News

Gavana Sonko aanika hali mbaya ya vyoo katika uwanja wa ndege wa JKIA ▷ Kenya News

Published

on


-Gavana Sonko alifika kwa ghalfa katika vyoo vya uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta na kuvipata vikiwa katika hali mbaya

– Vyoo hivyo havujakamilika na mteja lazima afanya ujuzi fulani ndiposa aweze kuvitumia ipasavyo

– Sonko alichukua video ya vyoo hivyo na kuonyesha jinsi vilivyokosa vifaa muhimu ya mteja kutumia baada ya kuenda haja ndogo

– Hata hivyo, Sonko amekuwa akikashifiwa kwa mazingira chafu jijini Nairobi ikiwemo vyoo chafu vya umma vilivyomo katikati ya jiji

Gavana wa Nairobi Mike Sonko alifika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta ghafla na kufululiza hadi kwenye vyoo vya wanaume.

Habari Nyingine: Naibu OCS wa Likoni ajiuwa baada ya kumuua mpenziwe kwa kumpiga risasi

Sonko aliweza kubaini kuwa vyoo hivyo vilikuwa katika hali mbaya na mteja lazima afanya ujuzi fulani ndiposa aweze kuvitumia vyoo hivyo ipasavyo.

Kulingana na video aliyoichapisha kwenye mtandao wa Facebook, Sonko alikashifu usimamizi wa kampuni hiyo kwa kuzembea kazini na kuweka afya wa wananchi hatarani.

Habari Nyingine: Mlemavu agusa nyoyo za wengi baada ya kuonekana akifanya maandamano dhidi ya unyakuzi wa ardhi

Habari Nyingine: Atwoli ajitetea kuhusu matamshi yake, akanusha uvumi kuwa alimtakia Ruto kifo

Aidha, Sonko alidai iwapo hatakuwa na uwezo wa kuzalisha tena, atashitaki kampuni ya ndege ya JKIA kwa mazingira duni hasa ya kudhuru afya ya binadamu.

Hata hivyo, Sonko amekuwa akikashifiwa na Wakenya kwa kufanya jiji la Nairobi kuwa na mazingira chafu jambo, ambalo kila mara yeye amekuwa akidai kulishughulikia.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO TV

Source: Kiswahili.tuko.co.ke

Source link

Comments

comments

Trending