Connect with us

General News

Hospitali ya Shalom yafunguliwa tena baada ya kufungwa kwa majuma 3 ▷ Kenya News

Published

on


Hospitali yenye utata ya Shalom iliyooko kaunti ya Machakos imefunguliwa tena baada ya kufungwa kwa muda wa majuma matatu

Hospitali hiyo ilifungwa kufuatia utepetevu kazini ambapo mtoto wa miezi saba alipoteza maisha yake baada ya kudungwa shindano ya Morphine kwa kiwango zaidi ya kile cha kawaida.

Kulingana na Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Huduma za Matibabu na Wataalamu wa meno KMPDB, Daniel Yumbya, hospitali hiyo ilifunguliwa baada ya kufanyiwa ukaguzi wa kina.

Habari Nyingine: Mpenzi wa mwanamuziki Rayvanny atangaza tarehe rasmi ya harusi yao

Hospitali ya Shalom yafunguliwa tena baada ya kufungwa kwa majuma 3
Source: Facebook

Habari Nyingine: Mhasibu mkuu wa serikali Edward Ouko kuondoka afisini

Yumbya alisema bodi yake imeridhishwa kabisa na kutimizwa kwa mapendekezo kadhaa waliotoa wakati hospitali hiyo ilipofungwa wiki mbili zilizopita.

Bodi hiyo ilihakikisha kwamba wale wanaojiriwa katika hosptali hiyo wamehitimu kimasomo na watakuwa wakifanyiwa ukaguzi wa mara kwa mara kubaini iwapo wanafanya kazi kulingana na wajibu wao.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO TV

Source: Tuko

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending