Connect with us

General News

Jalas amshambulia vikali mwanamuziki Ringtone, amsihi aepukane na sarakasi nyingi ▷ Kenya News

Published

on


Mcheshi maarufu na mtangazaji wa kituo cha redio cha Milele FM, Jalas amemtaka mwanamuziki wa nyimbo za Injili Ringtone Apoko aepukane na sarakasi za hapa na pale na badala yake azingatie taaluma yake ya uimbaji

Ushauri wa Jalas unatokea siku chache baada ya Ringtone kuwasihi wafuasi wake mitandaoni kumsaidia kupata mke atakayemuoa.

Habari Nyingine Isiolo: Jamaa hali mahututi baada ya kujaribu kujinyofoa mkuki

Habari Nyingine: Mwanamuziki Bahati adai mkewe anapenda pesa na ndio sababu anafurahia ndoa

Ringtone alidai amepekua kila mahali ila hajafanikiwa kupata kipendacho roho.

” Tafadhali Ringtone Apoko, hebu na uwache sarakasi nyingi na uangazie taaluma yako ya uimbaji, pia unapaswa kuacha kujiandikia barua za majuto, hebu na uendelee na uimbaji tafadhali,” Jalas alisema.

Itakumbukwa kuwa Ringtone aliwahi mnunulia aliyekuwa mke wa mwanamuziki Diamond Platinumz gari la aina ya Range Rover akidai anampenda sana na angempatia kama zawadi iwapo angekubali kuwa mkewe.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Tazama habari zaidi kutok TUKO TV

Source: Tuko

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending