Connect with us

General News

Jamaa amtunuku mkewe Mercedes Benz kama zawadi ya harusi yao ▷ Kenya News

Published

on

Loading...


Video moja imesambaa mitandaoni ikimwonesha bwana harusi akimtunuku bi harusi gari la kifahari wakati wa maankuli baada ya kufunga ndoa.

Jumatatu, Juni 10, mpiga picha wa maharusi hao Mrav Brown, alipakia video mtandaoni ambayo ilifichua taswira ya jinsi mambo yalivyokuwa wakati bwana harusi akimtunuku mkewe zawadi hiyo ya kifahari.

Habari Nyingine: Mwanamume, 45, aliyeunda barabara ya kilomita 2 kwa mikono yake anasaka jiko

Kwenye video hiyo, bwana harusi na rafiki zake waliomsimamia katika harusi hiyo wanaonekana wakisakata densi wakiwa wameshikila funguo za gari kabla ya kumwelekeza bi harusi nje na mumuewe kumkabidhi gari la Mercedes-Benz lililokuwa limeegeshwa.

Habari Nyingine: Washukiwa wa mauaji ya askofu aliyeuwawa Meru wawachiliwa huru

“Haya ni maajabu! Kumtunuku mkeo gari mpya la Mercedes C Class kama zawadi ya harusi! Brown alisema.

Video hiyo ilisambaa kwa kasi huku takriban watu 726 000 wakiitazama baada ya kupakiwa katika ukurasa wa Twitter.

Video hiyo aidha iliwasisimua wengi ambao waliachwa vinywa wazi kutokana na hatua aliyoichukua bwana harusi.

@LFC103_ alisema, “Mungu nimeona kile umewatendea wengine.”

Hata hivyo, baadhi yao walisema kwamba bi harusi hakuonekana kushangazwa na hatua hiyo hata baada ya kuliona gari hilo la kifahari.

“Bi harusi hakuoneana kushangazwa na zawadi hiyo hivyo basi ni ishara tosha kwamba kwake hili si jambo geni,”JoQueen alisema.

“Hapa huenda kuna jambo. Hata jinsi alivyomkumbatia baada ya kupokea funguo za gari. Sielewi. Lakini nawatakia kila la heri,” Djnabss alidokeza.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko

Source link

Loading...
Advertisement
Loading...
Loading...

Facebook

Loading...

Trending