Connect with us

General News

Jamaa katili amtupa mtoto wa miaka mitano kutoka orofa ya tatu baada ya kukataliwa na wanawake ▷ Kenya News

Published

on


Mwanamme wa umri wa miaka 24 amekamtawa baada ya kumtupa mvulana wa miaka 5 kutoka orofa ya tatu ya duka moja la bidhaa za jumla huko marekani.

Kwa mujibu wa jamaa huyo kwa jina Emmanuel Aranda, msukumo wa kutekeleza kitendo hicho ulitokana na hasira aliyokuwa nayo baada ya kukataliwa na wanawake kadhaa aliokuwa akiwavizia.

Kisa hicho kilitokea Ijumaa, Aprili 12 katika duka la mjini Minnesota, wakati wanawake hao walitaja sababu mbali mbali za kumkataa mwanamme huyo.

Habari Nyingine: Pasta aliyempagawisha mtoto wa miaka 7 na kumpapasa kwa vidole sehemu nyeti afikishwa kortini

Emmanuel Aranda alifichua nia yake ya kutaka kuua baada ya kukataliwa na wanawake kadhaa kwenye duka la Minnesota waliotaja sababu mbali mbali. Picha WSBTV
Source: UGC
Source: UGC

Ripoti za shirika la habari la Atlanta zilisema kuwa, mtoto huyo anauguza majeraha mabaya ya kichwani na mifupa kadhaa ambayo imevunjika baada ya kuanguka kutoka urefu wa kina cha futi 40 wa jumba hilo.

Kwa mujibu wa mamake mwathiriwa, Aranda alimsongea wakati akiwa ameketi pamoja na wanawake wengine nje ya mkahawa wa Rainforest Cafe.

Mwanamke huyo aliporajibu kumuuliza iwapo alitaka wampishe, jamaa huyo ambaye hakujibu lolote alimchukua mtoto huyo bila onyo na kumtupa kutoka orofa ya tatu walipokuwepo.

Hata hivyo Aranda alikamatwa papo hapo.

Mshukiwa alikiri kutekeleza unyama huo na kufichua kuwa siku iliyotangulia alikuja mahali hapo akiwa na nia ya kutaka kumuua mtu bila mafanikio.

Awali, alifichua kuwa alinuia kumuua mtu mzima lakini kwa kuwa njama yake ilienda kinyume na matarajio yake, aliamua kumuangamiza mtoto huyo.

Habari Nyingine: Jamaa apewa kichapo na mkewe kwa kukataa kumwambia ni mrembo

“Mshukiwa alidai kwamba, kwa miaka mingi amekuwa akija katika duka hilo kumtafuta mchumba lakini juhudi zake hazikwa zinazaa matunda kwani kila mara alikataliwa. Kila alivyokataliwa, alihisi machungu na kupandwa na mori,” mshtakiwa huyo alidai.

Inasemekana kuwa, Aranda alikuwa amepigwa marufuku dhidi ya kuzuru eneo hilo baada ya kupatikana na hatia ya kuwashambulia watu kadhaa katika matukio mawili tofauti 2015.

Kwenye kisa kimoja, mtuhumiwa alimrushia glasi ya maji na kisha baadaye ya chai mwanamke aliyedinda kumnunulia kitu alichokuwa akidai katika duka hilo.

Aidha kutokana na visa hivyo, Aranda aliamuriwa kufanyiwa uchunguzi wa kiakili kubaini iwapo yupo timamu.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Subscribe to watch new videos

Source: Kiswahili.tuko.co.ke

Source link

Comments

comments

Trending