Connect with us

General News

Johnstone Muthama adai Uhuru na Ruto wametengana kisiasa ▷ Kenya News

Published

on

Loading...


Aliyekuwa seneta wa Machakos Johnstone Muthama amedai kwamba Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto hawashirikiani tena katika huduma zao kwa wananchi.

Mwanasiasa huyo alipendekeza kuwepo kwa maombi ya kitaifa ili kuwaleta viongozi hao wawili na vile vile kupunguza joto la kisiasa nchini.

Habari Nyingine: Mwanga wa Kiswahili: Matumizi ya neno ‘kwa’

Johnstone Muthama adai Uhuru na Ruto wametengana kisiasa

Johnstone Muthama adai Uhuru na Ruto wametengana kisiasa. Picha: Nation
Source: UGC

Akizungumza huko Matungulu jimbo la Machakos mnamo Ijumaa, Julai 17, mwanasiasa huyo wa zamani alisema kwamba uhusiano baina ya Uhuru na Ruto uliharibiwa na Raila na Kalonzo.

“Matamshi ya Uhuru na Ruto hukinzana mara kwa mara. Wakati Raila anapowatubumia watu jukwaani matamshi yake yanaungwa mkono na Kalonzo. Ni wakati sasa wa kuomba kwa kuwa nchi inaelekea pabaya,” alisema.

Aliwasuta vikali viongozi na kusema kwamba wanafanya siasa kwa manufaa yao kibinafsi kupitia kushinikiza kwa kuleta mabadiliko kwa katiba.

Muthama amewataka Wakenya kukataa kushirikishwa katika mapendekezo hayo akidai kwamba ni njama ya wanasiasa kutaka kupambana na changamoto zinazowakumba binafsi.

Habari Nyingine: Mahakama yamwachilia huru jamaa aliyemjeruhi kwa kisu mkewe baada ya kumpata na mpango wa kando kitandani mwake

Muthama alidokeza kwamba wafuasi wa Ruto hususan kutoka Bonde la Ufa hawajafurahishwa na mwelekeo unaochukuliwa na wanasiasa na semi zao huenda zikazua vurugu miongoni mwa jamii zinazosihi eneo hilo.

“Ukiwasikia wanasiasa kutoka Bonde la Ufa wakimtetea Ruto, ni bayana kwamba semi zao haziungi mkono umoja. Semi zetu zinakinzana na huenda hilo likaleta vurugu nchini. Tunahitaji maombi,” Muthama aliongeza.

Loading...

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko.co.ke

Source link

Comments

comments

Loading...
Advertisement
Loading...
Loading...

Facebook

Loading...

Trending