Connect with us

General News

Joseph Hellon: Mumewe Esther Arunga alikuwa akitumia uchawi ▷ Kenya News

Published

on


Quincy Timberlake, mumewe aliyekuwa mwanahabari Esther Arunga alikuwa ni mchawi aliyetaka kubadili njia zake, mhubiri Joseph Hellon amesema.

Timberlake na Arunga walikuwa washirika wa Hellon katika kanisa la Finger of God kabla ya wawili hao kuondoka nchini Kenya huku maisha yao kuzongwa na a utata.

Habari Nyingine: Atwoli aonyesha penzi tamu, ampeleka mkewe Kilobi ughaibuni kusherekea ‘birthday’

Joseph Hellon pamoja na Esther Arunga na Quincy Timberlake. Picha: UGC
Source: UGC

Akiongea kwenye mahojiano na runinga ya NTV Julai 16, Hellon alisema Timberlake alikuwa amempasulia mbarika kuwa alikuwa ni mchawi lakini alitaka kuingia kanisani ili aokolewe.

“Quincy alikuwa akitumia mbinu za uchawi … na ninajua hayo kwa sababu aliniambia,” Hellon alisema.

Arunga alikutana na Timberlake kwenye kanisa la Hellon na penzi likaota kati yao.

Habari Nyingine: Afisa wa polisi apatikana ameuawa Thika baada ya kutoweka

Mhubiri Hellon alisema binti huyo alikuwa ni mtu msumbufu na alikataa kuskiza ushauri wake alipomwambia kuwa Quincy alikuwa anashiriki ushirikina.

Kwa sasa, wapenzi hao wawili wanazidi kupitia matatizo mengi nchini Australia ambapo wana kesi ya mauaji ya mtoto wao.

Tayari Arunga alikiri kwa maafisa wa polisi kuwa alikuwa ametoa habari za uongo kuhusu kilimuua mtoto wao ili kumlinda mume wake.

Kosa hilo huenda likafanya afungwe jela kwa kipindi cha hadi miaka ishirini.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending