Connect with us

General News

Kampuni ya Thiwasco yashirikiana na shirika moja la Denmark – Taifa Leo

Published

on


Kampuni ya Thiwasco yashirikiana na shirika moja la Denmark

NA LAWRENCE ONGARO

KAMPUNI ya maji ya THIWASCO imeanza mradi mkubwa wa maji wa Sh11 bilioni kwa lengo la kutosheleza wakazi kwa miaka mingi ijayo.

Shirika moja la kimataifa la Danish Sustainable Infrastructure Finance (DSIF), limefanya ushirikiano na kampuni ya THIWASCO ili kufanikisha mradi huo.

Makamu wa rais wa shirika hilo la DSIF, Tina Kollerup Hansen, alipongeza mpango huo akisema utatosheleza matakwa ya wakazi wa Thika kwa kupata maji kwa wingi.

Kulingana na mpango huo, baada ya mradi huo kukamilika, utaongeza lita 36 milioni za maji kwa siku.

Kwa jumla usambazaji wa maji utafika jumla ya lita 65 milioni kwa siku ikilinganishwa na lita 39 milioni ambazo hupatikana kwa wakati huu.

Ujumbe wa watu wanane kutoka Denmark ulizuru kampuni ya THIWASCO mnamo Alhamisi wiki jana kwa lengo wa kujionea wenyewe mpangilio uliowekwa kabla ya mradi huo kuzinduliwa rasmi.

“Tayari tumejionea mipango iliyowekwa na kampuni ya maji ya THIWASCO, ambapo tumeridhika nayo. Sasa kilichobaki ni kazi yenyewe kuzinduliwa,” alisema Hansen.

Alisema baada ya makubaliano tayari wamefikia sehemu muhimu ya maelewano ambapo kilichobakia sasa ni kazi kuanza.

“Huu ni mradi wa kujivunia kwani nchi ya Kenya itapata ujuzi wa hali ya juu kwa upande wa kiteknolojia huku wakazi wa Thika wakipata maji safi ya matumizi,” alifafanua Hansen.

Mkurugenzi wa kampuni ya THIWASCO, Mhandisi Moses Kinya, alipongeza juhudi za Shirika hilo Kwa kusema ni hatua kubwa ya kuokoa mahitaji ya wakazi wa THIKA.

Alitaja mto Chania na Thika kama maeneo muhimu yatakayotumika kwa mradi huo.

Alitaja maeneo matatu pia yatakayojengwa kwa kupitisha majitaka. Maeneo hayo ni Pilot, Nanga na Kilimambogo.

Alisema mradi huo pia utafanyika kupitia mradi wa Athi Water Works Development Agency.

Katika hafla hiyo, mkurugenzi huyo aliandamana na wakuu katika kampuni hiyo Mhandisi Joseph Kamau na wafanyakazi wengine katika maeneo tofauti.Source link

Comments

comments

Facebook

Trending