– Kibicho ndiye anapanga mkutano wa Rais Kenyatta na wabunge katika Ikulu ya Nyeri
– Tangatanga wamekuwa wakidai Kibicho anatumia wadhifa wake kumkandamiza DP Ruto
– Mkutano huo wa Rais umezua tumbo joto kwenye mrengo wa Tangatanga
Licha ya upinzani mkali kutoka kwa wabunge wa mrengo wa Tangatanga, katibu katika wizara ya Usalama wa Ndani Karanja Kibicho anazidi kung’aa na kujitokeza kama mmoja wa wanaoaminika na Rais Uhuru Kenyatta.
Haya yamebainika baada ya kujiri kuwa katibu huyo ndiye anapanga shughuli za mkutano wa faraghani kati ya Rais Kenyatta na wabunge kutoka Mt Kenya utakaofanyika Nyeri hii leo, Novemba 15.
Habari Nyingine: Pasta Ng’ang’a kupigana na shetani kanisani na taarifa zingine zilizopepea
Katibu katika wizara ya Usalama wa Ndani Karanja Kibicho ndiye anapanga mkutano wa faraghani kati ya Rais Kenyatta na wabunge wa Mlima Kenya. Picha: Standard
Source: UGC
Kulingana na gazeti la People Daily la Ijumaa, Novemba 15, Kibicho anapanga mkutano huo kupitia kwa utawala wa makamishna wa kaunti ambao wanawaalika viongozi wa kisiasa na kijamii kutoka kaunti za Mt Kenya kwenye mkutano huo.
Mutano huo utafanyika kwenye Ikulu ndogo ya Nyeri, Sagana.
Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung’wah alisema alipata mwaliko kutoka kwa kamishna wa Kiambu Wilson Wanyanga.
Ripoti za mkutano huo zilijiri Alhamisi, Novemba 14, lakini ajenda ya mkutano huo haijabainika wazi lakini mbunge mmoja aliambia TUKO.co.ke wanashuku siasa za Handisheki, 2022 na BBI ndio zitazungumziwa.
Habari Nyingine: Kakamega: Majambazi watoroka na kusahau bastola iliyokuwa imefungwa ndani ya chupi
Wabunge wa Tangatanga wamekuwa wakimlaumu Karanja Kibicho na kusema anatumika kuhujumu siasa za DP Ruto kuelekea 2022. Picha: Standard
Source: Facebook
Wabunge wa Tangatanga wamekuwa wakimlaumu katibu Karanja Kibicho na kusema anatumika kuhujumu siasa za Naibu Rais William Ruto kuelekea 2022.
Aidha baada ya uchaguzi wa Kibra, kundi la wabunge wanaomuunga mkono Ruto lilisema kuwa Kibicho na waziri Fred Matiang’i walitumika na kinara wa ODM Raila Odinga kwa kuwataka wafumbie jicho ghasia zilizoshuhudiwa.
Habari Nyingine: Sarah Cohen aomba mahakama aruhusiwe kufika kwake kuchukua mvinyo
Mkutano huo wa Mt Kenya umezua wasiwasi ndani ya mirengo ya Kieleweke na Tanga huku wakisubiri kusikia semi za Uhuru zitaegemea upande upi.
Awali, kulikuwa na uvumi kuwa ni wabunge wa mrengo wa Kieleweke pekee ambao walialikwa kwenye mkutano huo.
Hata hivyo, ilibainika kuwa viongozi wote kutoka kaunti za Mt Kenya watakuwemo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videos