Connect with us

General News

Kioja chazuka baada ya mke kumnasa mumewe na sindiria katika koti lake ▷ Kenya News

Published

on


Mlofa wa mtaa wa Lanet alipatwa na kigugumizi baada ya mkewe kumtaka amueleze ni vipi sindiria ilipatikana katika mfuko wa koti lake.

Inasemekana kuwa jamaa alikuwa na mazoea ya kufika nyumbani usiku wa manane akiwa mlevi chakari na wakati mkewe alijaribu kumdadisi kuhusu mienendo yake, polo alisema alikuwa akihudhuria ibada za kesha.

Habari Nyingine: Rais Uhuru Kenyatta amtembelea Mzee Moi hospitalini

Siku ya kisanga kwa mujibu wa Taifa Leo, polo alifika nyumbani kuchelewa akiwa mlevi chakari kama ilivyokuwa ada yake na hapo wakaanza kukorofishana na mkewe na kuwaamsha majirani.

Wakiwa katika hali hiyo, vita vikazuka baina yao huku mama akisemekana kumkaba mumewe shati kabla ya kumbwaga chini.

Habari Nyingine: Jukwaa la Malenga wa Ushairi

Katika harakati hiyo, mama alichomoa sindiria ndani ya mfuko wa koti la kalameni na kuwaacha majirani wakimaka kwa mshangao.

Mke alishuku mumewe ambaye alishindwa kujitetea alikuwa ametoka kujiburudisha na vimada usiku huo.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending