Connect with us

General News

Kipusa atokota baada ya vidosho kumparamia mpenziwe mzungu wakitaka urafiki ▷ Tuko.co.ke

Published

on


Mwanamke mmoja amezua kicheko mitandaoni baada ya kujitokeza na kuwakemea marafiki zake kwa kujaribu kumpokonya mpenzi wake.

Mwanadada huyo kwa jina Sistrin Rozette, aliwakemea swahiba zake ambao anadai wamekuwa wakimtumia mpenzi wake wa asili ya kizungu maombi ya urafiki katika Facebook, akiwataka waseme wazi wazi lengo lao la kutuma maombi hayo.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Habari Nyingine : Ezekiel Mutua amkosoa Linus Kaikai, asema serikali haina uwezo wa kuingilia Makanisa

Katika ujumbe aliounakili katika Facebook mnamo Alhamisi, Machi 21, Sistrin alidai kuwa ni yeye anayemiliki ukurasa wa mpenziwe hivyo basi ana uwezo wa kujua chochote kinachoendelea humo.

Kulingana na kipusa huyo, swahiba zake walivamia ukurasa wa mpenziwe huyo mzungu na hata kuanza kumtumia jumbe za maombi ya kutaka urafiki naye pindi tu alipotangaza kuwa wanachumbiana.

“Kila mtu yeyote anayemtumia jumbe za maombi ya urafiki mpenzi wangu ni sharti ajue kuwa ni mimi namiliki ukurasa wake na wangu,” mwanadada huyo aliandika.

Sistrin ambaye ni mkaazi wa Mombasa aliongeza kuwa, tayari anawajua wanaojaribu kumvizia mchumba wake ingawaje hatowaaibisha hadharani

“Kwa kuwa nawajua nyinyi nyote sitawataja. Chochote mnachotaka kumwambia mpenzi wangu naomba mniambie mimi, heshimuni uhusiano wetu jinsi mimi navyoheshimu wenu pia,” aliongeza.

Habari Nyingine: 11 wafariki katika ajali mbaya ya barabarani Kikopey

Hata hivyo ujumbe wake ulizua mgawanyiko baina ya wafuasi wake mitandaoni, baadhi wakionesha msisimuko wao huku wengine wakihoji kuwa ana haki ya kuutetea uhusiano wao na mpenziwe.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa inayoweza kubadilisha maisha ya mtu na ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690 na Telegram: Tuko news

Subscribe to watch new videos

Source: Kiswahili.tuko.co.ke

Source link

Comments

comments

Trending