Connect with us

General News

Kurunzi ya Lugha

Published

on


Kiswahili ni mojawapo ya lugha ambazo zinatumika katika mawasiliano haswa katika kanda ya Afrika mashariki. Lakini jambo ambalo watu wengi wameshindwa kung’amua ni maana ya lugha hii.

Lugha ni mfumo wa nasibu za ishara za sauti wenye maana unaotumiwa na wanadamu katika mawasiliano.

Katika lugha ya Kiswahili, kuna sifa ambazo zinatumika kuweza kuwa na mtiririko wa mawasiliano:

1. Lugha ya Kiswahili ni yenye mfumo

Kila lugha ina idadi maalum ya sauti inayotumia katika mawasiliano. Sauti hizi huunda maneno yanayosaidia katika mawasiliano.

Mfano: ‘Wewe utakuja kesho’ badala ya ‘utakuja kesho wewe’.

2. Ni ya Maana

Mpangilio wa sauti lazima uwe na maana.

Mfano: ‘Abab’ halina maana lakini ‘baba’ lina maana. Kwa hivyo kando na sauti maana pia huzingatiwa.

Habari Nyingine: Kurunzi ya Kiswahili: Madai Kiswahili ni lugha mseto hayana msingi

3. Inahusisha binadamu

Lugha hutumiwa tu na binadamu na hutofautiana na mawasiliano ya wanyama.

4. Hutumiwa kama chombo cha mawasiliano

Huwasaidia mahuluki kupashana habari kemkem hivyo kuwa chombo kizuri cha kupitisha ujumbe. Kando na kupashana basi pia wanakuwa na uelewano.

5. Lugha ni kioo cha jamii

Huangazia vitu, desturi, vitendo na matamanio ya adinasi waishio katika utamaduni fulani.

Taarifa nyingine: Mtangazaji Njambi Koikai afutilia mbali madai kuwa amefariki dunia

Umuhimu wa lugha ya Kiswahili

Kando na sifa, Kiswahili kina umuhimu nadhifu kwenye jamii.

 • Ni kitambulisho cha jamii: Huwatambulisha waja watokao katika janibu fulani hasa Afrika Mashariki.
 • Katika mawasiliano: Hutumiwa kupitisha ujumbe kutoka mtu mmoja hadi mwengine.
 • Ni lugha ya taifa kwa hivyo kutumiwa katika bunge la kitaifa katika vikao na mijadala mbalimbali.
 • Huleta uwiano: Huunganisha wananchi kwa kuwaleta pamoja kama lugha ya taifa.
 • Ni nguzo kubwa katika kuimarisha biashara hivyo kuendeleza biashara baina ya watu maanake kuna uelewano.
 • Kinaendeleza utamaduni katika jamii kwa kukipitisha kutoka kizazi kimoja hadi kingine hivyo kinakuza utamaduni.
 • Huendeleza kazi ya sanaa, hasa inapohusu kuwaelezea waja ujumbe muhimu.
 • Huweza kusuluhisha migogoro mbalimbali itokeapo kati ya waja kutoka tabaka tofauti tofauti hivyo kuleta muafaka.

Habari Nyingine: Bei ya petroli na mafuta taa yapanda

Changamoto zinazoikumba lugha ya Kiswahili

Lugha ya Kiswahili inapitia changamoto nyingi haswa katika karne hii ya 21 inayoendeshwa na teknolojia.

 • Upinzani kutoka lugha ambazo zilijitanua kama king’eng’e, kihispania, kifaransa kwa kuwa waja wengi wamejikita katika kuzizungumza lugha za kigeni.
 • Kukinasibisha na lugha ya kislamu. Madai kuwa Kiswahili ni lugha ya kiislamu yamewafanya wengi haswa wasio waislamu kutokipenda wakidai kuwa watakuwa wanazungumza lugha ya watu wengine.
 • Kiswahili kimechukuliwa kuwa lugha ya watu wa hali ya chini kitaaluma. Lakini, ukweli kubainika kuwa, watu walio na kisomo cha hali ya juu wanakipenda Kiswahili mno kuliko inavyodaiwa.
 • Matumizi ya lugha shaghalabagala ‘sheng’ hasa miongoni mwa vijana wa siku hizi ni changamoto kubwa sana kwani huku kuchanganya msimbo wa Kiingereza na Kiswahili umeleta kuchanganyikiwa kwa watumizi hivyo kuwawia muhali kuzungumza Kiswahili sanifu.

Makala yameandikwa na Jellys Wanzala.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending