Connect with us

General News

Mabasi 6 ya Modern Coast yenye abiria 90 yanaswa Sultan Hamud ▷ Kenya News

Published

on


Mamia ya abiria waliokuwa wakisafiri kwa mabasi mawili ya kampuni ya Modern Coast wamekwama mjini Sultan Hamud, kaunti ya Makueni Jumatano, Desemba 18 alfajiri baada ya polisi kunasa mabasi hayo.

Mabasi hayo yalikuwa yakisafiri kutoka mjini Mombasa kuelekea maeneo ya bara licha ya marufuku iliyowekwa dhidi yao na Mamlaka ya Usalama Barabarani (NTSA) wiki iliyopita.

Habari Nyingine:

Habari Nyingine:

Kila basi lilikuwa na abiria 45 wakati polisi wa trafiki walipoyasimamisha mwendo wa saa tisa na nusu alfajiri katika kizuizi cha barabara mjini Sultan Hamud kama aliyovyosema Kamanda wa Polisi Kaunti ya Makueni Joseph Ole Napeiyan.

Haya yanajiri siku chache baada ya leseni ya kampuni hiyo ya kuhudumu kupokonywa kufuatia ajali ya mabasi yake mawili kugongana eneo la Kiogwani katika barabara kuu ya Mombasa- Nairobi ambapo watu saba walifariki.

Habari Nyingine:

Watu wengine 60 walijeruhiwa vibaya katika ajali hiyo iliyotokea mwendo wa saa sita za usiku Jumatano, Desemba 12.

Kila moja ya mabasi yaliyonaswa yalikuwa na abiria 45 wakati maafisa wa polisi wa trafiki walipoyasimamisha katika kizuizi cha barabara mjini Sultan Hamud.

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending