Connect with us

General News

Magazeti ya Kenya Ijumaa, Novemba 15: Mkutano wa Rais Kenyatta watingisha ulingo wa siasa ▷ Kenya News

Published

on


1. The Star

Habari za mkutano wa Rais Uhuru Kenyatta na wabunge kutoka eneo la Mlima Kenya zimeshamiri kwenye magazeti ya Ijumaa.

Kulingana na gazeti la The Star, Rais Kenyatta atakuwa anakutana na kikosi cha wabunge ambao wamekuwa wakitoa semi za kupinga jopo la uwiano BBI kwenye mkutano huo utakaofanyika Sagana, Nyeri.

Mkutano huo utawaleta pamoja viongozi wote kutoka eneo la Mlima na umezua joto la kisiasa haswa ndani ya mirengo ya Kieleweke na BBI.

Gazeti la The Star limeangazia mkutano wa Rais huko Sagana Nyeri kama nafasi ya kukutana na waasi wa BBI. Picha: Julius Otieno
Source: Facebook

2. Standard

Gazeti la Standard vile vile limeangazia habari za mkutano wa Sagana kwenye kura yake ya kwanza.

Wahariri wa gazeti hilo wamechukua msimamo wa kuwa mkutano huo uliitishwa ili Rais Kenyatta aweze kuwazima wabunge ambao wanamfuata DP Ruto kwa kile limesema ni kuzima vuguvugu linalosababisha wimbi la kumfuata DP.

Gazeti hilo pia lina taarifa kuhusu dawa za kupanga uzazi ambazo zinamaliza makali yako kitandani na kufanya ushindwe kushiriki kitendo.

Magazeti ya Kenya Ijumaa, Novemba 15: Mkutano wa Rais Kenyatta watingisha ulingo wa siasa

Baadhi ya mbinu za kupanga uzazi zinawafanya kina mama kupoteza hamu ya penzi la ndoa. Picha: Julius Otieno
Source: Facebook

3. People Daily

Kando na taarifa kuhusu mkutano wa Rais Kenyatta ambao umefanya ulingo wa siasa kusaga meno, gazeti hili linafuatilia taarifa kuhusu kizungumkuti kinachozunguka jamaa aliyeanguka kutoka kwa ndege ya KQ huko Uingereza mwezi Juni.

Kituo cha habari cha Sky News kilichapisha taarifa na kusema kimebaini jamaa huyo ni mkenya kwa jina Paul Manyasi kutoka Kakamega.

Sky News walisema walikuwa wamezungumza na familia moja iliyokiri kuwa Manyasi alikuwa mtoto wao aliyekuwa akifanya kazi katika uwanjwa wa ndege wa kimataifa wa JKIA na alitoweka mwezi Juni.

Hata hivyo, hayo yamebadilika na familia kukana taarifa hizo pamoja na picha zlizodaiwa kuwa za Manyasi kuibuka kwenye mtandao na jina tofauti.

Magazeti ya Kenya Ijumaa, Novemba 15: Mkutano wa Rais Kenyatta watingisha ulingo wa siasa

Kizungumkuti kinazunguka kisa cha jamaa aliyeanguka kutoka kwenye ndege ya KQ iliyokuwa karibu kutua Uingereza kutoka Nairobi. Picha: Julius Otieno
Source: Facebook

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690.

Subscribe to watch new videos

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending