Connect with us

General News

Makali ya njaa Turkana: Nanok ampongeza Sonko kwa ukarimu wake kuokoa watu ▷ Kenya News

Published

on


– Kaunti ya Turkana ndiyo inayoubeba mzigo mkubwa we baa la njaa ambao umesababishwa na ukame wa muda mrefu

– Sonko alijitolea na kuandamana na msafara wa magari ya vyakula vya msaada alivyotoa kwa ajili ya watu wanaoteswa na makali ya nja Turkana na Pokot Magharibi

– Seneta wa Turkana Malik Ekai aliwaomba viongozi wengine wenye nia njema kuchukua mfano we Sonko

Gavana wa Turkana Josephat Nanok amempongeza mwenzake we Nairobi Mike Sonko kwa ukarimu wake kuwasaidia wakaaji eneo lake wanaokabiliwa na njaa.

Sonko alipeleka chakula cha msaada Turkana na Pokot Magharibi, Kaunti ambazo familia zimeubeba mzigo mkubwa wa makali hayo ya njaa.

Habari Nyingine: Washukiwa walionaswa na pesa bandia katika benki ya Barclays wafikishwa mahakamani

Nanok alimpongeza sana Balozi huyo wa Matendo Mema, na kusema taji alilopewa na shirika moja la Israeli linamfaa vyema kwa sababu ya matendo yake. Picha: Mike Sonko/Twitter
Source: Twitter

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Msafara wa magari ya chakula ulifika Turkana Jumapili, Machi 24, na Sonko aliandamana nao na kabla ya zoezi la kuanza kugawa chakula hicho alifanya mashauriano na mwenyeji wake.

Nanok alimpongeza sana Balozi huyo wa Matendo Mema, na kusema taji alilopewa na shirika moja la Israeli linamfaa vyema kwa sababu ya matendo yake.

Habari Nyingine: Chama cha Raila chapanga njama ya kumfurusha Naibu Rais William Ruto afisini

“Nataka kusema asante sana Sonko. Ni zaidi ya rafiki kwetu. Naamini jukumu la kuwa Balozi wa Matendo Mema ni haki yako. Tunashukuru kwa vyakula ulivyotuletea,” Nanok alisema.

Sonko alisema kuleta kwake chakula hicho sio siasa

“Hatuko hapa kwa ajili ya kupiga siasa. Tunafahamu karibia kaunti 13 zinakabiliwa na njaa na tutaendelea na kuzifikia,” alisema.

Habari Nyingine: Murang’a: Mwanafunzi wa kidato cha 3 aliuliwa kinyama, mwili watupwa mtoni

Miongoni mwa vyakula alivyopeleka ni unga wa mahindi, mafuta ya kupikia, maziwa, kabeji, viazi, matikiti maji, machungwa na vyakula vinginevyo ikiwamo mboga.

Mwakilishi we Kike Turkana Joyce Emarikor na Seneta Malik Ekai walimpokea Sonko na kuwataka viongozi wengine wenye nia njema kuiga mfano we gavana huyo we Nairobi.

Maeneo kulikopelekwa chakula ni Kerio Delta, Lochwa, Kaptir,Loima, Gold, Lotikipi, Kamarese, Kerio, Nakukulas, Lojere Emoit, Kadeli na Katioko miongoni mwa maeneo mengine.

Habari Nyingine: Wanandoa chokoraa waliuza vifaa vyote vya nyumba, wakakataa ajira – Mpiga picha Muchiri

Mbali na kupeana chakula cha msaada, kundi la Sonko Rescue Team liliweka kambi ya matibabu Tobong ambapo mamia ya watu walihudumiwa.

Viongozi wengine waliokuwapo ni Jeremiah Lomorka (Loima), Mohamed Ali, (Turkana Mashariki), James Lomenen (Turkana Kusini), John Lodepe (Turkana Ya Kati), Christopher Nakuleu (Turkana Kaskazini) miongoni mwa wengine.

Ripoti ya Dan Ole Muhuni – Ripota wa TUKO.co.ke

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Kiswahili.tuko.co.ke

Source link

Comments

comments

Trending