Connect with us

General News

Mama na mtoto wapokea shahada katika chuo kimoja ingawa walisomea vyuo tofauti ▷ Kenya News

Published

on


Sharonda Wilson na mtoto wake wa kiume Stephan wote wamepata shahada kutoka Chuo Kikuu cha Central Michigan, eneo la Mlima Pleasant, Marekani, baada ya kupanga kukosa sherehe ya kufuzu kwake na badala yake kuhudhuria ya mwanawe katika Chuo Kikuu cha Serikali cha Ferris.

Mama kwa jina Sharonda Wilson na mwanawe, Stephan wamepata shahada kutoka Chuo Kikuu cha Michigan ya Kati, eneo la Mlima Pleasant, Marekani, baada ya kupanga kukosa sherehe ya kufuzu kwake na badala yake kuhudhuria ya mwanawe.

Sharonda alikuwa akitarajia kupata Stashahada yake kutoka Chuo Kikuu cha Serikali cha Ferris kilichopo Big Rapids, Michigan.

Habari Nyingine: Gavana wa Jubilee sasa aonya Kenya huenda ikatawaliwa na Mchina

Mwanawe, Stephan pia alikuwa akihitimu siku hiyo katika Chuo Kikuu cha Michigan ya Kati katika eneo la Mlima Pleasant, na hivyo aliona bora kukosa hafla yake na badala yake ahudhurie ya mwanawe.

Lakini Sharonda alipokuwa akipanga hivyo, chuo chake na kile cha mwanawe vilikuwa na mpango tofauti.

Siku chache kabla ya hafla hiyo, Wilson aliandika kupitia Facebook kuhusu masaibu yake na mmoja wa watu waliouona ujumbe wake ni mwanafunzi anayefanya kazi katika ofisi ya rais Michigan ya Kati.

Habari Nyingine: Mambo yabadilika: Raila Odinga ajipata pabaya Muhoroni, wafuasi wamkemea vikali wakimtaja kuwa msaliti

Asubuhi ya Jumamosi, siku ya hafla ya kuhitimu, mwanafunzi huyo alimfahamisha rais, Bob Davies, kuhusu suala hilo na alichukua hatua ya kushauriana na mwenzake wa chuo cha Ferris, David Eisler.

Davies alitaka kufahamu ikiwa chuo cha Eisler kingeweza kumpa Wilson shahada yake.

“Kila kitu kiligeuka mara moja,” Ari Harris, msemaji wa Chuo Kikuu cha Michigan ya Kati, alifichua.

Sharonda na Stephan walipokea vyeti vyao katika Chuo Kikuu cha Michigan ya Kati.

Habari Nyingine: Tanzania: Wezi walioiba dhahabu, pesa nyumbani kwa Reginald Mengi wakamatwa

Stephan Wilson, ambaye ni mmoja wa kundi la watumbuizaji muziki katika chuo hicho walifanikisha sherehe hiyo kwa vibao mbalimbali.

Mto alielezea furahaya yake kuh wakufuzu wakati mmoja na mama yake mzazi na siku hiyo atakuwa akiikumbuka maisha yake yote.

“Nimekuwa nikitazamia kwa muda mrefu kupokea shahada yangu, muda mrefu,” Stephan alisema.

Aliongeza kuwa, ”kupata shahada hii ni hatua kubwa maishani mwangu, na kuwa na mama kusherehekea hafla hii ni baraka kubwa. Nina fahari kubwa kwetu wote.”

Habari Nyingine: Ruto anukuu mstari wa Bibila kwa ufasaha siku chache baada ya kukosea

Wilson alipata shahada ya Sayansi katika Usimamizi wa Biashara, na mtoto akapata shahada ya Sanaa katika Muziki.

Davies, aliwapongeza wawili hao kwa mafanikio yao na kusema walistahili.

“Sharonda na Stephan wote walitia bidii na wanafaa kusherehekea pamoja kama familia,” Davies alisema katika ujumbe wake kwa wawili hao. “Tunashukuru kwa ushirikiano wetu na marafiki zetu Ferris kufanikisha hafla ya pamoja ya Stephan na Sharonda.”

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko Kenya

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending