Connect with us

General News

Manchester City wazamisha chombo cha Manchester United ligini – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Manchester City wazamisha chombo cha Manchester United ligini – Taifa Leo

Manchester City wazamisha chombo cha Manchester United ligini

Na MASHIRIKA

MANCHESTER City walikung’uta majirani zao Manchester United 2-0 katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) na kumweka kocha Ole Gunnar Solskjaer katika presha ya kupigwa kalamu ugani Old Trafford kwa mara nyingine.

Japo kichapo kutoka kwa Man-City ambao ni mabingwa watetezi wa EPL hakikuwa kinono sawa na kile cha 5-0 ambacho mashetani wekundu wa Solskjaer walipata kutoka kwa Liverpool mnamo Oktoba 24, kilichokuwa dhahiri ni kwamba Man-United walizidiwa maarifa katika takriban kila idara.

Kufikia sasa, Man-United wameshinda mechi tano, kuambulia sare mara mbili na kupoteza michuano minne kati ya 11 iliyopita. Matokeo hayo yamewazolea alama 17, sita nyuma ya Man-City wanaonolewa na kocha Pep Guardiola. Man-City watavaana na Everton, Paris Saint-Germain (PSG) na West Ham United katika mechi tatu zijazo. Wameshinda mechi saba, kutoka sare mara mbili na kupoteza michauno miwili kati ya 11 zilizopita ligini.

Man-City walifungua ukurasa wa mabao kunako dakika ya saba kupitia Eric Bailly wa Man-United aliyejifunga baada ya presha kutoka kwa Joao Cancelo. Bao hilo liliwapa City motisha na wangalifunga mabao zaidi ila mengi ya makombora kutoka kwa Cancelo, Gabriel Jesus na Kevin de Bruyne yalidhibitiwa vilivyo na kipa David de Gea.

Bernardo Silva alifunga goli la pili la Man-City baada ya kuwazidi maarifa mabeki Harry Maguire na Luke Shaw. Kombora la pekee ambalo Man-United walielekeza langoni mwa Man-City katika kipindi cha kwanza lilitokana na juhudi za Cristiano Ronaldo aliyebanwa vilivyo katika vipindi vyote viwili vya mchezo.

Man-United walishuka dimbani kwa minajili ya gozi hilo wakijivunia rekodi ya kupepeta Man-City mara tatu, kutoka sare mara mbili na kupoteza mara moja katika mechi sita zilizopita ligini ugani Trafford.

Ilikuwa mechi ya 49 kukutanisha vikosi hivyo ligini na ya 186 katika historia. Baada ya kuvaana na Watford ligini mnamo Novemba 20 ugani Vicarage Road, Man-United watarudiana na Villarreal katika Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) kabla ya kumenyana na Chelsea, Arsenal na Crystal Palace mtawalia. Mechi hizo zitakuwa mtihani mkubwa ambao huenda ukaamua mustakabali wa Solskjaer ugani Trafford.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO