Connect with us

General News

Mariga akumbana na kizingiti kingine tena dhidi ya kuwania ubunge wa Kibra ▷ Kenya News

Published

on

Loading...


– Kinyanjui alisema utaratibu na kanuni za chama hazikuzingatiwa kabla ya Jubilee kumwidhinisha Mariga kama mgombea wake

– Haya yanajiri siki moja tu baada ya IEBC kumkabidhi Mariga cheti cha kuwania ubunge wa Kibra

– Mariga amekumbwa na changamoto si haba tangu Jubilee alipopokezwa tikiti ya kuipeperusha bendera ya Jubilee Kibra

Nyota wa soka McDonald Mariga apata pigo tena kuhusiana na azma yake ya kuwania kiti cha ubunge cha Kibra kwenye uchaguzi utakaofanyika Novemba 7, 2019.

Hii ni baada ya kesi nyingine kuwasilishwa mbele ya jopo la kutatua mizozo ya vyama kupinga kuchaguliwa kwa Mariga na chama cha Jubilee.

Mariga akumbana na kizingiti kingine tena dhidi ya kuwania ubunge wa Kibra

Mariga alipokezwa cheti cha kuwania unbunge Kibra na IEBC Septemba 16, 2019. Picha: The Star
Source: UGC

Habari Nyingine: Kachero Jane Mugo ajitokeza, kufikishwa mahakamani Jumatano

Kwenye kesi hiyo, Kinyanjui amesema kuwa zoezi la kumchagua mgombea atakayeipeperusha bendera ya chama cha Jubilee haikufuata sheria na kanuni za chama.

Mlalamishi huyo alisema kuwa ameusikitikia uamuzi wa IEBC kumpa nyota huyo wa zamani wa soka cheti cha kuwania kiti cha Kibra kwani anaamini kanuni za chama hazikuzingatiwa kabla ya kuchaguliwa kwake.

Habari Nyingine: Esther Passaris asema upasuaji aliofanyiwa na daktari umefanikiwa

Aliitaka bodi hiyo kuyasikiza malalamishi yake na kutoa uamuzi kabla ya tarehe ya uchaguzi huo.

Loading...

Awali, Mariga alikuwa amefungiwa nje ya uchaguzi kwa tuhuma kwamba alikuwa hajasajiliwa kama mpiga kura katika eneo la Kibra.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.

Source link

Comments

comments

Loading...
Advertisement
Loading...
Loading...

Facebook

Loading...

Trending