Connect with us

General News

Mbunge wa Shinyalu Justus Kizito akiri hadharani yeye ni ‘fisi’ ▷ Kenya News

Published

on


Mbunge wa Shinyalu Justus Kizito aliwashangaza wananchi baada ya kukiri hadharani kuwa yeye huvutiwa na vipusa warembo na hufanya kila awezalo kuwatongaza na kisha kuwachumbia

Kizito aliwasuta wakosoaji wake wanaodai yeye huwapotosha wanawake wengi kwa kujinufaisha kingono bila kuzingatia kwamba yuko na mke na familia.

Habari Nyingine: Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo akanusha madai ya Raila Odinga kuzomewa Muhoroni

Akizungumza akiwa eneo mbunge la Shinyalu, Kizito alishangazwa ni vipi wanaume wanakuwa na machungu anapopendwa na vipusa warembo ilhali kila mwanaume aliumbwa amtamani mwanamke.

” Hebu waniambie eti ni mwanamke amelalama eti nilimlazimisha kushiriki naye ngono, iwapo hawajui kuwatongoza wanawake na kuwafanya wafurahie maisha, basi wanapaswa kuachana na mimi kabisa,” Kizito alisema.

Habari Nyingine: Raila adai vyombo vya habari viliwapotosha Wakenya kuhusu SGR Macharia: SGR lazima itafika Kisumu

Mbunge wa Shinyalu Justus Kizito akiri hadharani yeye ni ‘fisi’
Source: Facebook

Habari Nyingine: Habari njema kwa walimu wasiokuwa na ajira, serikali inapanga kuajiri 95 elfu

Kizito alitoa madai hayo baada ya picha zake kadhaa kuenezwa mitandaoni akiwa na vipusa warembo kwenye eneo la burudani, jambo lililowaghabisha baadhi ya viongozi kutoka eneo bunge lake.

” Nilikuwa kwenye hafla moja mjini Nakuru ambapo nilikutana na wanawake wawili walioniomba nipigwe picha nao, mimi kuwakumbatia sikuwa na nia mbaya ila wakosoaji wangu wakawA wepesi kuifanya ionekane kana kwamba nilikusudia jambo mbaya,” Kizito alisema.

Baadhi ya wakaaji walielezea wasiwasi wao kwamba Kizito yuko na mazoea ya kuwatongoza wasichana wenye umri mdogo na kwa wale hutafuta ajira, lazima ashiriki nao ngono ndiposa awasaidie.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO TV

Source: Tuko

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending