Connect with us

General News

Miguna Miguna: Uhuru anamchezea Raila karata ya siasa ▷ Kenya News

Published

on


– Mageuzi ya kikatiba ni ya kuinufaisha familia ya Kenyatta kulingana na Miguna Miguna

– Raila anatumiwakisiasa ili katiba ibadilishwe lakini atatupwa nje ya serikali baada ya miezi sita

– Wakili Miguna amewataka Wakenya kukataa mageuzi ya katiba

Mwanaharakati Miguna Miguna amesema Rais Uhuru Kenyatta anamchezea karata ya siasa Raila Odinga.

Miguna alisema kuna njama inayopangwa na familia ya Rais Kenyatta na ile ya rais mstaafu Daniel Moi kuendelea kushikilia uongozi lakini wanataka kumtumia kiongozi wa ODM Raila Odinga kufanyia katiba mageuzi ili lengo lao liafikiwe.

Hata hivyo, mwanasiasa huyo matata anadai baada ya familia hizo kuafikia lengo lao, basi Raila Odinga atatupwa nje ya serikali.

Habari Nyingine: Khalwale ampongeza Matiang’i kwa kuwafurusha wamiliki haramu wa kampuni za kamari

Miguna Miguna amewataka Wakenya kukataa mageuzi ya katiba. Picha: Miguna Miguna/Facebook
Source: UGC

Kwenye mtandao wake wa twitter, Miguna aliweka uchanganuzi wake wa ‘njama’ hiyo inayonuia vile vile kumtumia kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka.

Wakili huyo aliye nchini Canada alisema mikakati iliyoko kwa sasa ni katiba ibadilishwe ili Rais Kenyatta aendelee kushikilia wadhifa wake, Raila awe waziri mkuu huku seneta wa Baringo Gideon Moi akifanywa naibu rais.

Habari Nyingine: Jubilee haikuwa ya kushinda uchaguzi

Lakini alionya kiongozi huyo wa ODM kuwa kwenye mfumo huo wa serikali, atafurushwa baada ya miezi sita kwani wandani wa Kenyatta watamsingizia kuhusu jambo fulani serikalini na kupata nafasi ya yeye kufurushwa.

“Raila atateuliwa waziri mkuu asiye na mamlaka na Gideon Moi naibu rais, baada ya miezi sita, Raila atasingiziwa kuhusu ufisadi na kutolewa kwenye wadhifa huo na kupewa mtu kutoka chama cha KANU,” Miguna alisema.

“Kenya itafanywa taifa linaloongozwa na mtu mmoja. Taifa litakalokuwa likiongozwa na familia za Kenyatta na Moi,” aliongeza.

Miguna alichukua nafasi hiyo kuwataka Wakenya kukataa wito wa kubadilisha katiba.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko.co.ke

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending