General News
Mike Sonko amtaka Gavana Waiguru ajifungue katika hospitali ya Pumwani ▷ Kenya News
Gavana Mike Sonko Jumapili, Julai 14, aliwasha moto kwenye mtandao wake wa Instagram baada ya kudai kuwa Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru ni mjamzito.
Waiguru alifunga pingu za maisha na mpenzi wake wakili Kamotho Waiganjo Jumamosi Julai 13 na siku moja tu baada ya sherehe hiyo ya iliyonoga huko Kirinyaga, Sonko alidai wawili hao wanatarajia kujifungua hivi karibuni.
Habari Nyingine: DP Ruto achemka baada ya taarifa Tuju anapangia Raila mikakati ya 2022
“Kabla hata ya fungate ianze, nachukua nafasi hii kwa niaba ya familia yangu na wakazi wa Nairobi kwa mwenzangu kutoka Kirinyaga Anne Waigruu kwa kuoana na Wakili Waiganjo,” Sonko alisema.
“Na ninakutakia hali salama wakati wa kujifungua mtoto wenu aliye njiani,” aliongeza Sonko.
Habari Nyingine: William Kabogo awaonya wanasiasa dhidi ya kuzungumzia mauaji ya Kiambaa
Wengi walishangaa iwapo ni kweli Gavana Waiguru ni mjamzito ama ni sarakasi tu za Gavana Sonko.
Hili lilichanganya zaidi baada ya mwanasiasa huyo ambaye amejipa umaarufu kutokana na mitindo yake ya mavazi na sarakasi mitandaoni aliposema hata mke wake atajifungua kwenye hospitali hiyo ya akiina mama ya Pumwani.
“Unakaribishwa kujifungua katika hospitali ya akina mama ya Pumwani … hata mke wangu anatarajiwa kujifungua katika hospitali hiyo katika miezi michache ijayo,” Sonko aliongeza.
Gavana Sonko ni mmoja wa magavana ambao hawakuhudhuria harusi ya Waiguru licha ya viongozi wakuu serikalini akiwemo Rais Uhuru Kenyatta, na viongozi wa upinzani Raila Odinga na Kalonzo Musyoka kufika kwenye sherehe hiyo.
Naibu Rais William Ruto vile vile hakuhudhuria dhifa hizo.
READ ENGLISH VERSION
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news
Source: Tuko
var FBInitEvent = new Event('fb:init');
document.dispatchEvent ? document.dispatchEvent(FBInitEvent) : console.warn('dispatchEvent is not supported')
window.FB.Event.subscribe('edge.create', function(response) { if (window.Site.fbLiked && (window.Site.fbLiked instanceof Function)) { window.Site.fbLiked(); } }); }; }
(function(d, s, id){
var js, fjs = d.getElementsByTagName(s)[0];
if (d.getElementById(id)) {return;}
js = d.createElement(s); js.id = id; js.async = !0;
js.src = "http://connect.facebook.net/en_US/sdk.js";
fjs.parentNode.insertBefore(js, fjs);
}(document, 'script', 'facebook-jssdk'));
Source link
-
General News6 days ago
We have no home, say survivors of West Pokot landslide : The Standard
-
Entertainment5 days ago
Mike Sonko: Kipchumba Murkomen, Mutula Kilonzo Junior among Nairobi governor’s lawyers ▷ Kenya News
-
Trending Videos7 days ago
DP Ruto urges leaders to take common stand on BBI implementation
-
General News4 days ago
Government lays conditions for vetting private security firms : The Standard
-
Politics3 days ago
Senator Kipchumba Murkomen on the spot(VIDEO) – Weekly Citizen
-
Entertainment2 days ago
WATCH: World’s Tallest Building Lights Up In The Colours of Kenya’s National Flag
-
Entertainment4 days ago
Opinion: Sonko will not be jailed, the system is on his side ▷ Kenya News
-
Tech5 days ago
Jumia Kenya is downsizing| Starts banner advertising to bolster revenues