Connect with us

General News

Mkewe Bahati awasha mitandao na picha za kuvutia zikimuonyesha ujauzito wake ▷ Kenya News

Published

on


Mwanamuziki wa nyimbo za injili Kevin Bahati na mkewe Diana Marua walisisimua mitandao ya kijamii Jumatano Mei 15 baada ya kutangaza kuwa wanatarajia mtoto wao wa pili

Kupitia picha kadhaa alizozichapisha kwenye mitandao ya kijamii, Bahati alimpongeza mkewe kwa kuwa mjamzito na kumshukuru Mungu kwa kumbariki mara kwa mara.

Habari Nyingine: Mzungu awaanika peupe vipusa wa Kenya, asema wanalazimisha mahaba

” Nimekuwa nikifanya kazi sana kitandani, namshukuru Mungu kwa kunibariki tena, hebu na mmtumie Diana jumbe za pongezi,” Bahati aliandika Instagram.

Mwanamuziki huyo alitangaza habari hizo njema akiwa nchini Dubai ambapo alikuwa wamekwenda na mkewe kwa ajili ya likizo.

Habari Nyingine: CCTV: Jamaa mwenye ‘tattoo’ aonekana kwa Wangari usiku aliouawa

Wafuasi wao walifurika mitandaoni na kuwatakia kila la heri wanandoa hao hasa wanaposubiri kuzaliwa kwa malaika wao.

Diana na Bahati wameoana kwa miaka mitatu na kwa pamoja wamejaliwa mtoto msichana, Heaven Bahati ambaye kwa sasa yuko na umri wa wa mwaka mmoja.

Habari Nyingine: Alichosema afisa wa magereza kwenye mtandao kabla ya kuuawa

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO TV

Source: Tuko.co.ke

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending