Connect with us

General News

Msafiri mlevi akojolea mkoba wa abiria mwenzake, akamatwa na kutiwa mbaroni ▷ Kenya News

Published

on


Polisi wamemtia mbaroni msafiri mmoja aliyedaiwa kuwa mlevi baada ya kukojolea mkoba wa msafiri mwenzake wakiwa katika ndege.

TUKO.co.ke imebaini kuwa ndge hiyo ilikuwa inasafiri kutoka Chicago eneo la Charlotte na ilitarajiwa kutua saa 12.52 asubuhi mnamo, Alhamisi, Machi 2.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Habari Nyingine: Nabii David Owuor alitabiri kuhusu tetemeko la ardhi iliyofanyika Kenya Jumapili Machi 24

Msafiri mlevi aliyejisaidia kwenye mkoba wa mwanamke akamatwa. Picha:www.americanairlines.co.uk
Source: UGC

Kulingana na shirika la Daily Mail, picha ya msafiri huyo mtundu haijatolewa rasmi baada ya kitendo hicho kilichofanyika nchini Marekani siku ya Alhamisi, Machi 21.

Kulingana na taarifa za polisi, wahudumu wa ndege hiyo waliwajuza maafisa wa polisi kuhusu kitendo hicho na kuwataka kumtia mbaroni jamaa huyo aliyekuwa mlevi pindi ndege hiyo itakapotua.

Habari Nyingine: Raila atoa onyo kali kwa Ruto kuhusiana na vita dhidi ya ufisadi

Kufikia sasa taarifa kumhusu muathiriwa wa tukio hilo zinaonesha kuwa ni msafiri wa kike, na kitendo hicho kiliripotiwa katika kituo cha Federal Bureau of investigations (FBI).

Hata hivyo haijabainika wazi kuhusu adhabu mshukiwa huyo atapewa.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa inayoweza kubadilisha maisha ya mtu na ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690 na Telegram: Tuko news.

Subscribe to watch new videos

Source: Kiswahili.tuko.co.ke

Source link

Comments

comments

Trending