Connect with us

General News

Msanii Kambua atangaza kuwa ni mja mzito baada ya miaka mingi ya kutafuta mtoto ▷ Kenya News

Published

on


Msanii wa nyimbo za injili ambaye pia alikuwa mtangazaji wa kipindi cha Kubamba ni mja mzito, TUKO.co.ke imemaini.

Kambua aliwashangaza mashabiki wake baada ya kutangaza katika ukurasa wake mtandaoni kuwa alikuwa mja mzito.

Habari Nyingine: Shoga Mkenya George Barasa amumezea mate hadharani jamaa mzungu kwenye

Kwenye ujumbe aliouchapisha Instagram mnamo Ijumaa, Mei 17, msanii huyo alipakia picha yake akiwa ameshikilia tumbo lake ambalo lilionekana kweli ‘limefura.’

Kufuatia tangazo hilo, watu mashuhuri kama vile Grace Msalame, Sheilla Mwanyigha, Hopekid, Pitson, Alice Kamande na wengine walimtumia jumbe za kumpongeza kwa mwamko mpya.

Wafuasi wake aidha hawakuwachwa nyuma, kwani walifurika katika ukurasa wake pia na kumtakia kila la heri.

Kwa muda mrefu, msanii huyo amekuwa akishambuliwa mitandaoni kwa ajili ya ‘kutokuwa’ na uwezo wa kupata mwana na mumewe licha ya kuishi katika ndoa kwa miaka mingi.

Kambua hata hivyo aliwanyamazisha waliokuwa wakimshambulia kwa kuchapisha jumbe mitandaoni, akisema kuwa alimtumainia Mwenyezi Mungu kwa baraka hiyo ambayo alisema itatimia kwa wakati ufaao.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko.co.ke

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending