MGOMBEAJI urais wa chama cha Democratic Party Justin Muturi, ameonya vyama vidogo dhidi ya miungano kadhaa ya kisiasa kabla ya uchaguzi mkuu wa Agosti 9.
Bw Muturi ambaye pia ni spika wa Bunge la Taifa, alisema vyama vidogo vya kisiasa havifai kulazimishwa kujiunga na miungano inayoibuka lakini vinafaa kuruhusiwa kujijenga mashinani na kunawiri hadi siasa za kitaifa.