Connect with us

General News

Mume asimulia jinsi mke alivyomdunga mtoto wao kisu – Taifa Leo

Published

on


Mume asimulia jinsi mke alivyomdunga mtoto wao kisu

MWANAMKE wa umri wa miaka 28 anayedaiwa kumdunga kisu mtoto wake wa mwaka mmoja, alikuwa ametishia kumuua mtoto huyo, mahakama ya Eldoret iliambiwa Alhamisi.

Babake mtoto alimweleza Hakimu Mkaazi Mkuu wa Eldoret Christine Menya kwamba mshtakiwa mara kadhaa alitishia kumuua mtoto huyo.

“Kabla ya tukio hili, mshtakiwa, ambaye ni mke wangu, alinitishia kwamba siku moja angemuua mtoto wangu,” aliambia mahakama.

Mahakama iliambiwa kwamba kabla ya tukio hilo wanandoa hao wamekuwa wakizozana kinyumbani na kusababisha mtoto huyo kudhalilishwa.Mtoto huyo alidungwa kisu upande wa kushoto na kumjeruhi utumbo wake.

Akitoa ushahidi katika kesi hiyo, daktari kutoka Hospitali ya Rufaa ya Moi (MTRH) aliambia mahakama kuwa kutokana na majeraha aliyopata mtoto huyo, bado amelazwa katika kituo hicho kutokana na maambukizi ya kudungwa kisu.

Afisa wa upelelezi aliwasilisha suruali iliyolowa damu ambayo mtoto huyo alikuwa amevalia wakati wa kisa hicho pamoja na kisu ambacho kinadaiwa kilitumiwa.

Welmah Jepkemboi alitenda kosa hilo katika nyumba yake iliyoko Kipkaren mjini Eldoret mnamo Agosti 16, 2022.

Bi Jepkemboi alishtakiwa kusababisha madhara ya kudumu kinyume na kifungu cha 234 cha Kanuni ya Adhabu.

Shtaka lilisema kuwa mshtakiwa alitumia kisu cha jikoni kumdunga mtoto wake wa mwaka mmoja.

Ripoti ya uchunguzi iliyopo mahakamani inaonyesha kuwa tukio hilo lilichochewa na ugomvi wa muda mrefu wa kinyumbani kati ya mshtakiwa na mumewe.Mtoto huyo aliokolewa na majirani ambao walimkimbiza hadi MTRH kwa matibabu.

Alikanusha mashtaka.

Tangu wakati huo mahakama imekataa kumwachilia kwa dhamana kutokana na ripoti ya awali ya dhamana kutoka kwa maafisa wa kurekebisha tabia.

“Kufikia sasa mahakama inasitasita kumwachilia mshtakiwa kwa bondi kutokana na ripoti ya kurekebisha tabia ambayo haimpendelei. Ataendelea kukaa rumande,” aliagiza hakimu.

Mshtakiwa atajua kama ana kesi ya kujibu Januari 24, 2023.Source link

Comments

comments

Facebook

Trending