Connect with us

General News

Mwanamke adai alikula uroda na shemejiye akidhani ni mumewe bila kujua ▷ Kenya News

Published

on


-Mfanyibiashara kwa jina Kudirat Ajayi amefichua kwamba alifanya mapenzi na shemejiye

-Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 52 alidai kwamba alidhani shemejiye alikuwa bwanake

-Ajayi alikiri hayo baada ya mumewe kuwasilisha kesi mahakamani ya kutaka talaka

Mfanyabiashara aliyetambulika kama Kuditat Ajayi kutoka Afrika Kusini, ameimbia mahakama kwamba alishiriki ngono na shemejiye akidhani alikuwa mumewe.

Mumewe Ajayi alikuwa amewasilisha kesi mahakamani akiomba kutalakakiana na mkewe.

Habari Nyingine: Picha za kupendeza za mtangazaji Doreen Majala akisherehekea siku yake ya kuzaliwa

Hata hivyo, mwanamke huyo alidai kwamba shemejiye aliwasili nyumbani kwao usiku wa manane na alimtambua tu baada ya kushiriki mapenzi naye kulingana na Briefly.

“Nilikuwa katika chumba chetu cha kulala wakati shemeji yangu alifika nyumbani usiku na kuingia chumbani humo. Nilidhani alikuwa mume wangu kwani yeye ana mazoea ya kuja nyumbani saa za usiku na tunashiriki mapenzi kisha tunalala. Nilibaini alikuwa ni shemeji yangu pindi tu baada yake kufanya mapenzi na naye. Nilipomuuliza alidai kwamba alilala na mimi sababu mme wangu alikuwa amesafiri,” mwanamke huyo alisema.

Aliongeza kwamba alimshtaki jamaa huyo kwa wifi yake ambaye alimshauri asimfichulie yeyote kuhusu kisa hicho kwa ajili ya kuwepo kwa amani katika familia.

Habari Nyingine: Wakenya waorodhesha mahari ya kuchukiza walioagizwa na wakwe zao

Kulingana na mfanyibiashara huyo, mumewe amekuwa anawapa malezi bora zaidi wana wa wake zake wengine kuwaliko wanao.

Mwanamke huyo alikana mashtaka hayo na kuiomba mahakama kuitupilia mbali kesi hiyo kwa kuwa alikuwa angali anampenda mumewe.

Hata hivyo jamaa alishikilia kukamilika kwa ndoa yao hiyo huku akimshutumu mkewe kwa kuwa mzinifu akidai kwamba alipata mtoto mmoja nje ya ndoa.

Habari Nyingine: Passaris atofautiana na Sonko baada ya ubomozi wa Pangani

“Wakati nilipomuoa, nilimkodishia nyumba kwa kuwa nina wake wengine ambao sikutaka waishi pamoja. Nilianza kupata fununu kutoka kwa majirani kwamba mke wangu alikuwa na uhusiano na mwanamme mwingine ila nilipuuza hadi pale ambapo mpenzi wake huyo alianza kudai kwamba mmoja wa watoto wetu ni wake.

“Hatimaye mwanamme huyo aliamua kuja nyumbani lakini nilikataa kumfungulia mlango. Wakati nilipomuuliza mke wangu, alikiri kufanya mapenzi na jamaa huyo ila hakupata mimba,” Akande aliiambia mahakama.

Hakimu wa mahakama hiyo, Adeniyi Koledoye, aliwataka wawili hao kutulia na kusitisha uhasama baina yao hadi pale ambapo kesi hiyo itakapoamuliwa Alhamisi, Agosti 22.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko.co.ke

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending