Connect with us

General News

Mwanamuziki Vivianne akana madai kuwa alishiriki ngono na mbunge Jaguar ▷ Kenya News

Published

on


Mwanamuziki maarufu Vivianne amekanusha madai kuwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mbunge wa Starehe Charles Njagua almaarufu Jaguar

Kupitia ujumbe mrefu alouchapisha Instagram, Vivianne alisema Jaguar amekuwa mshauri wake mkuu wa kimziki na amemsaidia kukuza talanta yake ya uimbaji.

Habari Nyingine: Kirinyaga: Kalameni alia mke anaringa baada ya kuteuliwa kwenye kamati ya kanisa

Madai haya yanaibuka baada ya baadhi ya wafuasi wake kumkashifu kwa kushiriki ngono na mbunge huyo ambaye pia ni star wa muziki anayemiliki studio za Main Switch.

” Sijawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Jaguar wala kushiriki ngono naye kama vile inavyodaiwa na baadhi ya wafuasi wangu, Jaguar ni mshauri wangu wa kimziki na amenisaidia sana kukuza talanta yangu ya uimbaji,” Vivianne alisema.

Habari Nyingine: Gavana Lee Kinyanjui amteua naibu wake kuwa waziri wa barabara

Kulingana na Vivianne, Jaguar amemsaidia sana hasa kwa kukuza miziki zake na kumfanya kuwa maarufu hasa alipofanya collabo naye.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko.co.ke

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending