Connect with us

General News

Mwanamuziki wa miziki ya Pop Adele atangaza kutengana na mumewe Simon Konecki ▷ Kenya News

Published

on


Msanii wa miziki ya aina ya pop Adele ametengana na mumewe ambaye wameishi naye kwa miaka nane, Simon Kanocki.

Taarifa hiyo ilitangazwa rasmi Ijumaa, Aprili 19, na wawakilishi wake Adele, Benny Tarantini na Carl Fysh.

Habari Nyingine: Zari Hassan atangaza kupata mchumba mwengine

Hata hivyo, msanii huyo na mumewe watashirikiana katika kumpa malezi mwanao wa kikume mwenye umri wa miaka 6 ambaye walijaaliwa 2012.

“Adele ametengana na mumuwe. Aidha, wametangaza kujitolea kumlea mwanao na kumuonesha mapenzi ipasavyo. Hata hivyo wanaomba maamuzi yao yaheshimiwe hivyo basi hamna taarifa zaidi itakayotolewa,” wawili hao walisema.

Wachumba hao walifunga ndoa iliyokuwa na usiri mkubwa mno, lakini baadaye Adele alitangaza rasmi kuhusu tukio hilo mwaka wa 2017 akiwa katika tamasha moja.

Habari Nyingine: Moyo wa Pasaka: Wafanyabiashara wa Jua Kali wafanya usafi Kitale

Kwa wakati mmoja akipokea tuzo la Grammy, Adele pia alimtangaza Konecki kama mumewe ingawaje kwa mara nyingi, amekuwa akiyaficha mambo mengi kuhusiana na uhusiano wao.

Konecki ni mwanzilishi wa shirika la Life water na vile vile Drop4drop, ambalo linahakikisha kuwepo na kusambazwa kwa maji safi kote duniani.

Msanii huyo kutoka Tottenham alifunga ndoa na Konecki mwaka wa 2016 baada ya kuchumbiana kwa muda wa miaka mitano.

Adele alitoa albamu yake ya kwanza kwa jina 19 mwaka wa 2018, iliyokuwa na nyimbo kama Chasing Pavements na Hometown Glory, ambazo zilifanya vyema zaidi na kushikilia nafasi ya kwanza Uingereza.

Adele aidha, alitoa albamu nyingine, 25, mwaka wa 2015, iliyokuwa na wimbo wa Hello ambao ulimpa umaarufu zaidi duniani.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Subscribe to watch new videos

Source: Kiswahili.tuko.co.ke

Source link

Comments

comments

Trending