Connect with us

General News

Mwigizaji nyota wa Afro- Sinema, John Dumelo afanya harusi ya kukata na shoka ▷ Kenya News

Published

on


Mwigizaji maarufu wa filamu za Nollywood, John Dumelo hatimaye ameuasi ukapera

Dumelo na kipenzi chake walifanya harusi ya kufana iliyohudhuriwa na marafiki, jamaa na wageni waalikwa pekee.

Mwigizaji huyo ambaye yuko na maelfu ya wafuasi wa kike mitandaoni, alichapisha picha kadhaa za sherehe ya harusi yake na bila shaka ilikuwa ya kukata na shoka.

Bibi harusi alivalia gauni ya kipekee yenye bei ghali kwa mwonekano tu na ambayo ilimuonyesha umbo lake la kuvutia.

Walioomfanyia vipodozi bibi harusi pia walikuwa wataalamu katika urembo, walimfanya kipusa huyo angae kweli kweli.

Dumelo mwenyewe hakuachwa nyuma, alivalia suti maridadi aina ya tuxedo, tamanio la kila mwanamke.

Source: Tuko.co.ke

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending