Mwigizaji nyota wa Afro – Sinema kutoka Nigeria Regina Daniels alihudhuria tamasha la kuwakumbuka watoto wasiojiweza ambalo pia lililohudhuriwa na wasanii mashuhuri nchini Nigeria
Hata hivyo, imebainika kuwa, mmoja wale waliohudhuria tamasha hilo ni mpenzi wa zamani wa mwigizaji huyo, Adinma Sonma.
Haya yanajiri siku moja tu baada ya Regina kuolewa kitamaduni na mumewe wa miaka 59 ambaye pia anatambulika kuwa tajiri mkubwa nchini Nigeria.
Kupitia kwenye video ambayo imeenezwa mitandaoni Regina anaonekana akiwa na wakati mzuri na mpenzi wake wa zamani huku wakibadilishana vinywaji vya bei ghali.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.