Connect with us

General News

Nabii David Owuor alitabiri kuhusu tetemeko la ardhi iliyofanyika Kenya Jumapili Machi 24 ▷ Kenya News

Published

on


– Mtumishi wa Mungu alieleza kuwa alitabiri kuhusu tetemeko hilo la ardhi alipokuwa Peru

– Aliwaomba Wakenya kutubu ili wasiangamizwe na tetemeko la ardhi

– Wafuasi wake walijawa furaha wakieleza kuwa utabiri wa naabii wao ulitimia

Kiongozi wa kanisa la Holiness and Repentance nabii David Owuor amejitokeza na kueleza kuwa utabiri wake kuhusu tetemeko la ardhi Kenya umetimia baada ya tetemeko hilo kufanyika Jumapili, Machi 24.

Inadaiwa kuwa Owuor alitabiri kuhusu tetemeko hilo miezi sita iliyopita alipokuwa Peru, Kusini mwa Merikani.

Tuma neno ‘NEWS’ kwa 40227 ili kupata habari muhimu pindi zinapochipuka

Habari Nyingine: Tena: Uhuru aomba mkopo wa KSh 368 bilioni kutoka Uchina kukamilisha mradi wa SGR

Katika ujumbe uliochapishwa matandaoni muda mfupi baada ya tetemeko hilo mwendo wa 7pm Jumapili, Owuor alidai kuwa tukio hilo lilikuwa njia ya kuwakumbusha Wakenya kuwa wanastahili kutubu na kuwaheshimu ”manabii’’.

‘’ Tetemeko hili la ardhi ambalo nabii mkuu wa Mungu alilitabiri miezi sita iliyopita alipokuwa Peru ni njia ya kulikumbusha taifa la Kenya kutubu na kuwaheshimu manabii wakuu,’’

Habari Nyingine: Murang’a: Mwanafunzi wa kidato cha 3 aliuliwa kinyama, mwili watupwa mtoni

‘’ Mungu alinituma kuwaambia Wakenya kutemngeneza njia kwa manabii wakuu na kutubu bila hiyo, taifa lote litazamishwa na tetemeko la ardhi’’ Nabii Owuor alisema, kulingana na chapisho.

Habari Nyingine: Jamaa ajiua Kakamega baada ya kushindwa kulipa madeni

Kama ilivyoripotiwa awali na jarida la TUKO.co.ke, maeneo mengi ya Kenya yalishuhudia tetemeko hilo lilofanyika kwa sekunde kadhaa ila hakuna uharibifu ulioripotiwa.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa inayoweza kubadilisha maisha ya mtu na ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690 na Telegram: Tuko news.

Subscribe to watch new videos

Source: Kiswahili.tuko.co.ke

Source link

Comments

comments

Trending