Connect with us

General News

Ndoa mpya yatatiza mahesabu ya Ruto – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Ndoa mpya yatatiza mahesabu ya Ruto – Taifa Leo

Ndoa mpya yatatiza mahesabu ya Ruto

Na BENSON MATHEKA

NDOA ya kisiasa kati vyama vya Amani National Congress (ANC) na United Democratic Alliance (UDA), huenda ikavuruga hesabu za Naibu Rais William Ruto huku uchaguzi mkuu wa Agosti 9 unapokaribia.

Mnamo Jumapili, Dkt Ruto na kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi walitangaza ushirikiano wa vyama vyao unaolenga kumshinda kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga anayeungwa mkono na Rais Uhuru Kenyatta kupitia Azimio la Umoja.

Wawili hao hawajafichua mkataba wanaosema watawasilisha kwa msajili wa vyama vya kisiasa, na wadadisi wa siasa wanasema kwamba huenda ndoa ya kisiasa isichangamkiwe na viongozi na wapigakura wa Mlima Kenya ambao wanatarajia naibu rais kuteuliwa mgombea mwenza kutoka eneo lao.

Miongoni mwa washirika wa Dkt Ruto kutoka Mlima Kenya waliopigiwa upatu kuteuliwa mgombea mwenza ni mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua, mwenzake wa Kangema Alice Wahome na Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru ambaye ametangaza kuwa atatetea kiti chake.

“Uteuzi wa mgombea mwenza bila shaka utavuruga hesabu ya Dkt Ruto. Akikosa kuteua mgombea mwenza kutoka eneo la Mlima Kenya, atapoteza kura za eneo hilo ambalo litahisi amelisaliti. Akikosa kuteua Mudavadi, hatapata kura za eneo la Magharibi anazomezea mate,” anasema mchanganuzi wa siasa Joseph Musila.

Anasema ndoa yake ya kisiasa na Bw Mudavadi inapigwa darubini Wakenya wakitaka kuona iwapo atamteua kuwa mgombea mwenza wake, jambo ambalo linawezekana ikizingatiwa viongozi hao wawili wanapanga kuandaa mikutano ya kampeni pamoja.

Wachanganuzi wa siasa wanasema ni vigumu kwa wagombea urais wanaoshindana kuandaa mikutano ya pamoja ya kampeni jinsi Dkt Ruto na Bw Mudavadi wanavyopanga kufanya.Akizungumza Jumapili katika Bomas of Kenya, Nairobi, Dkt Ruto alitoa ratiba ya mikutano ya pamoja ya UDA, ANC na Ford Kenya ya Moses Wetang’ula kuanzia Nakuru, Kakamega na eneo la Kati ya nchi.“Kuanzia sasa tutatembea pamoja na Jumatano (kesho) tutakuwa Nakuru kabla ya kuzuru Magharibi Ijumaa na eneo la Kati mnamo Jumamosi,” Dkt Ruto alitangaza.

Bw Musila anasema kinachoweza kudumisha umaarufu wa Dkt Ruto eneo la Mlima Kenya ni kumfadhili Mudavadi kugombea urais kisha ateue mgombea mwenza kutoka eneo hilo.

“Akifanya hivi, anaweza kugawa kura milioni 2.2 za kaunti nne za Magharibi (Kakamega, Busia, Bungoma na Vihiga) ambazo zimekuwa zikimfaidi Bw Odinga katika chaguzi zilizotangulia na azoe sehemu kubwa ya kura milioni sita za eneo la Mlima Kenya iwapo hali haitabadilika kabla ya uchaguzi mkuu ujao, miungano ya kisiasa inaopoendelea kuibuka,” asema.

Kulingana na Prof Gitile Naituli wa Chuo Kikuu cha Multimedia, kama wagombeaji wengine wa urais, suala la mgombea mwenza litamkosesha usingizi Dkt Ruto hasa baada ya ukuruba wake mpya na Bw Mudavadi.

Anasema kuwa chaguo la mgombea mwenza litaongeza zaidi au kubomoa umaarufu ambao Dkt Ruto amejenga kwa miaka minne eneo la Kati tangu alipotofautiana na Rais Kenyatta.

Washirika wa Dkt Ruto eneo la Mlima Kenya wanasema hata baada ya kumkumbatia Bw Mudavadi, wanatarajia ateue mgombea mwenza kutoka eneo lao.

Seneta wa kuteuliwa Isaac Mwaura anasisitiza kuwa mgombea mwenza wa Dkt Ruto lazima atoke eneo la Mlima Kenya.

“Sisi katika Mlima Kenya tuna msimamo thabiti kwamba ni lazima mgombea mwenza ( wa Dkt Ruto) atoke eneo letu na msimamo huo haujabadilika,” Bw Mwaura alisema Jumatatu asubuhi.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending