Connect with us

General News

Nyamira: Serikali ya Kaunti yagundua wafanyakazi hewa 1000 katika sajili yake ▷ Kenya News

Published

on


– Kaunti ya Nyamira imegundua kuwapo wafanyakazi hewa 1000 katika sajili yake baada ya ukaguzi ambao wamekuwa wakipokea mishahara kila mwezi

– Ukaguzi huo ulitokana na malalamishi kutoka kwa wakazi walioshangaa ni kwa nini huduma hazitolewi inavyostahili wakati idadi ya wafanyakazi wa kaunti hiyo ni kubwa

– Gavana Nyagarama anajiandaa kufika mbele ya Kamati ya Seneti kuhusu matumizi ya pesa za umma, kuhojiwa kuhusu matumizi ya pesa katika mwaka wa fedha wa 2018/2019

Serikali ya Kaunti ya Nyamira imegundua kuwapo wafanyakazi hewa 1000 katika sajili yake ambao wamekuwa wakipokea mishahara kila mwezi.

Sasa wafanyikazi hao wa vitengo mbalimbali wataathirika baada ya majina yao kuondolewa kutoka katika sajili ya wafanyakazi wa kaunti hiyo inayoongozwa na Gavana John Obiero Nyagarama.

Habari Nyingine: Magezeti ya Kenya Ijumaa, Mei 17: Rais Mustaafu Daniel Moi atozwa faini ya KSh 1B

Kaunti ya Nyamira imegundua kuwapo wafanyakazi hewa 1000 katika sajili yake baada ya ukaguzi ambao wamekuwa wakipokea mishahara kila mwezi. Picha: UGC
Source: UGC

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya ukaguzi wa sajili hiyo ili kuwatambua halali na wale walioajiriwa bila utaratibu wa sheria pamoja na uwezo wa kutekeleza majukumu.

Ukaguzi huo ulitokana na malalamishi kutoka kwa wakazi pamoja na viongozi mbalimbali wa Nyamira walioshangaa ni kwa nini huduma hazitolewi inavyostahili wakati idadi ya wafanyakazi wa kaunti hiyo ni kubwa.

Habari Nyingine: Foleni ndefu zashuhudiwa katika vituo vya kusajili Huduma Namba

Nyamira: Serikali ya Kaunti yagundua wafanyakazi hewa 1000 katika sajili yake

Gavana Nyagarama anajiandaa kufika mbele ya Kamati ya Seneti kuhusu matumizi ya pesa za umma, kuhojiwa kuhusu matumizi ya pesa katika mwaka wa fedha wa 2018/2019. Picha: UGC
Source: UGC

Upatikanaji wa huduma umeripotiwa kuwa changamoto kubwa hali ambayo imechangia kukosekana maendeleo eneo hilo tangu serikali za kaunti kuanza kufanya kazi mwaka wa 2013.

Kufuatia ukaguzi huo, ilibainika wazi kwamba wafanyakazi wengi wamekuwa wakipokea mishahara licha ya kutofika kazini na kutokuwa na majukumu rasmi yanayoonekana.

Tukio hilo limesababisha maafisa wakuu wa wizara ya fedha katika serikali ya Nyagarama kupewa likizo ya lazima ili uchunguzi wa kina kufanywa.

Habari Nyingine: Kisumu: Gavana Nyong’o taabani kwa kutumia pesa za umma kuomba Raila msamaha

Hata hivyo gavana ameapa kuhakikisha kwamba wale wote waliohusika watafikishwa mahakamani na kushtakiwa.

Katika ripoti ya hivi majuzi kutoka kwa ofisi ya Waziri wa Ugatuzi Eugine Wamalwa kuhusu maendeleo katika kaunti mbalimbali, kaunti ya Nyamira ilikuwa miongoni mwa zinazoshika mkia.

Hayo yanajiri wakati Gavana Nyagarama akijiandaa kufika mbele ya Kamati ya Seneti kuhusu matumizi ya pesa za umma, kuhojiwa kuhusu matumizi ya pesa katika mwaka wa fedha wa 2018/2019.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending