Connect with us

General News

Okutoyi aduwazwa na mnyonge Australia, asema ni funzo – Taifa Leo

Published

on


Okutoyi aduwazwa na mnyonge Australia, asema ni funzo

Na GEOFFREY ANENE

NYOTA Angella Okutoyi amesema anachukulia kubanduliwa kwake mapema kwenye shindano la tenisi la chipukizi la J1 Traralgon nchini Australia mnamo Jumamosi ni funzo kwake.

Okutoyi, 17, ambaye anakamata nafasi ya 60 kwenye viwango bora vya Shirikisho la Kimataifa la Tenisi (ITF), aliduwazwa na nambari 431 Yilin Yan,16, kwa seti mbili bila jibu za 6-2, 6-2 katika mechi ya raundi ya kwanza.

Mechi hiyo ilikatizwa Ijumaa katika seti ya kwanza wakati Okutoyi alikuwa chini 4-2 kwa sababu ya mvua na radi kabla ya kuendelea mapema Jumamosi.

“Sikuanza mchuano huu vyema Ijumaa kitu ambacho kilimpa mpinzani wangu uongozi. Leo (Jumamosi) nilicheza vyema, lakini naye pia alikuwa mzuri zaidi. Nitachukua pigo hili kuwa funzo,” alisema Okutoyi ambaye shindano lake lijalo ni pia ni la chipukizi la Australian Open mnamo Januari 22-29.

Bingwa huyo wa Afrika wa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18 analenga kumaliza 2022 katika mduara wa 30-bora duniani.