Connect with us

General News

Picha za punde za Ken Okoth anayepata nafuu Ufaransa, mke wake zawafurahisha Wakenya ▷ Kenya News

Published

on


– Picha hizo zilichapishwa na Mwakilishi wa Kike Kaunti ya Nairobi Esther Passaris aliyemtembelea Okoth nchini France

– Wakenya walifurahishwa na picha hizo kwani mbunge huyo alionekana kuimarika kiafya zaidi

– Mbunge huyo alisema atapambana hadi kushinda vita dhidi ya ugonjwa wa saratani anaougua

Mbunge wa Kibra Ken Okoth ni mwenye afya nzuri inayoimarika kila siku, ikiwa picha ambazo TUKO.co.ke imezitizama ni za kuaminika.

Hali ya afya ya mbunge huyo imekuwa ikiimarika kila kukicha baada ya kuanza kupokea matibabu ya kukabiliana na saratani na Wakenya wanafurahia kumuona alivyo sasa hasa baada ya picha kuibuka tena mtandaoni Jumapili, Mei 19 akiwa katika afya tele na tabasamu kubwa.

Habari Nyingine: Sossion v Magoha: Walimu kwa njia panda huku wakipokea maagizo kinzani kuhusu mtaala mpya

Katika picha hizo, mbunge huyo amesimama na mke wake na Mwakilishi wa Kike wa Kaunti ya Nairobi, Esther Passaris wakiwa nchini Ufaransa anakoendelea (Okoth) kupokea matibabu..

Passaris mwenye furaha kubwa na ambaye alizichapisha picha hizo, alimpongeza Okoth kwa kumruhusu amtembelee hospitalini.

Habari Nyingine: Aisha Jumwa motoni baada ya kumlinganisha Ruto na Yesu

”Salamu kutoka kwa Mhe. Okoth Kenneth na mke wake Monica. Asante mheshimiwa kwa kutenga muda wako kunipokea leo. Nafahamu una hamu ya kurejea nyumbani na kuanza tena kazi. Sote tunaomba na kukutakia nafuu!” mwakilishi huyo aliandika kupitia Twitter.

Kufuatiaujumbe wake, Wakenya walichangia kwa jumbe za mbalimbali na kumshukuru Mungu kwa ajili ya afya ya Okoth ambayo imeimarika.

Habari Nyingine: Tajiri awalipia wanafunzi wa chuo kikuu deni la KSh 4 bilioni ili wafuzu

Wengi walikuwa na furaha kubwa kumwona mbunge huyo akiwa katika afya iliyoimarika na mwenye tabasamu kubwa wakati huu akiendelea kupokea matibabu kudhibiti saratani.

Ilivyoripotiwa awali na TUKO.co.ke, mbunge huyo aligunduliwa kuwa na ugonjwa huo miezi kadhaa iliyopita na bila ya uoga akatangaza kupambana na ugonjwa huo hadi kuushinda.

Read ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko.co.ke

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending