Connect with us

General News

PSG watandika Brest na kufungua pengo la alama 11 kileleni mwa jedwali la Ligue 1 – Taifa Leo

Published

on


PSG watandika Brest na kufungua pengo la alama 11 kileleni mwa jedwali la Ligue 1

Na MASHIRIKA

PARIS Saint-Germain (PSG) walikomoa Brest 2-0 mnamo Jumapili na kufungua pengo la alama 11 kati yao na nambari mbili Nice kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1).

PSG walitandaza mchuano huo bila kujivunia hudumza za wanasoka wao matata Lionel Messi anayeugua Covid-19 na Neymar Jr ambaye bado hajapona jeraha.

Mbappe aliwaweka PSG kifua mbele katika dakika ya 32 kabla ya Thilo Kehrer kuzamisha kabisa chombo cha wageni wao. Bao la Mbappe lilikuwa lake la 19 msimu huu na la 10 katika Ligue 1. Goli la Kehrer lilikuwa lake la pili kutokana na mechi 70 za Ligue 1.

PSG sasa hawajashindwa katika michuano 12 mfululizo ligini. Hata hivyo, ushindi dhidi ya Brest ulikuwa wao wa pili kutokana na mechi sita zilizopita.

Mbali na Neymar na Messi, wanasoka wengine waliokosa kuunga kikosi cha PSG ni beki Achraf Hakimi na kiungo Idrissa Gueye wanaowakilisha mataifa yao ya Morocco na Senegal mtawalia kwenye fainali za Kombe la Afrika (AFCON) zinazoendelea nchini Cameroon.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGOSource link

Comments

comments

Facebook

Trending