Connect with us

General News

Raila anajihusisha sana na shughuli za chama sio siasa za urithi 2022 – ODM ▷ Kenya News

Published

on


Chama cha ODM kimesema kuwa kinara wake Raila Odinga anajihusisha sana na masuala ya chama hicho na kwamba hana haja na siasa za urithi za uchaguzi mkuu wa 2022.

Chama hicho kilisema Raila hana mpango wowote wa kushiriki katika uchaguzi mkuu wa 2022 kwani yuko na mambo mengi yakutekeleza ndani ya chama chake.

Habari Nyingine: Kurunzi ya Kiswahili: Ni nini maana ya lugha ya Kiswahili?

Kupitia ujumbe uliochapishwa kwenye mtandao wa Twitter Jumatatu Mei 20, chama hicho kilisema Raila yuko mbioni kukiimarisha na amekuwa akihudhuria mikutano huku akipatiana ushauri katika chama hicho.

” Tunataka wananchi wajue kuwa kiongozi wetu wa chama cha ODM Raila Odinga anajihusisha sana na masuala ya chama na hana haja ya kujihususha na siasa za urithi 2022,” Ujumbe wa chama hicho ulisoma.

Habari Nyingine: Fahamu faida 25 za kufanya mazoezi

Haya yanajiri baada ya baadhi ya wafuasi wa Raila kulalama kuwa kiongozi huyo amekimya sana na kuwasilisha wasiwasi wao kwamba huenda siasa za 2022 ndizo zinampotezea wakati.

Kama iliyoripotiwa wali, chama cha ODM kilikiri kuwa kinakumbwa na matatizo ya kifedha na ndio sababu shughuli mingi zimesimamishwa.

Read: ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Tazama habari zaidi TUKO TV

Source: Tuko News

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending