Connect with us

General News

Raila Odinga ajipata pabaya Muhoroni, wafuasi wamkemea vikali wakimtaja kuwa msaliti ▷ Kenya News

Published

on


-Wakaazi wanapinga kujengwa kwa kiwanda na serikali

-Raila aliwataka wakubali radi huo unaofadhiliwa na serikali kuu

-Wakaazi walisema hawatakubali shamba lao litumiwe huku wakimwita Raila msaliti

Kiongozi wa ODM Raila Odinga amejipata pabaya huko Muhoroni baada ya wafuasi wake kumkemea huku wakipinga ujenzi wa kiwanda katika eneo hilo.

Utata ulianza alipowataka waruhusu ujenzi wa kiwanda hicho kwenye mashamba yao.

Raila aliwaambia ujenzi huo utakuwa wa manufaa kwao kushinda ukulima wanaofanya kwa sasa.

Habari Nyingine: Tanzania: Wezi walioiba dhahabu, pesa nyumbani kwa Reginald Mengi wakamatwa

Kiongozi huyo ambaye ana ufuasi mkubwa wa kisiasa eneo hilo alikuwa amelizuru mnamo Jumatatu, Mei 13, kuwataka wakaazi waruhusu ujenzi huo.

Hata hivyo, hilo halikukubalika huku vijana wakiandamana na kubeba mabango yaliomsuta Raila kwa kile walisema ni kuwasaliti.

“Kwa nini mnaniaibisha? Mimi nataka kuwaletea maendeleo ili mfaidike lakini hamuoni hilo,” Raila alisema akiwa mwingi wa fedheha.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko.co.ke

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending