Connect with us

General News

Rais Uhuru awavunja mbavu Wakenya ▷ Kenya News

Published

on


Rais Uhuru Kenyatta aliwaacha Wakenya kwenye mitandao wakiangua kicheko Jumapili, Mei 19, baada ya video yake yenye ucheshi kuibuka mtandaoni.

Kwenye video hiyo fupi, Uhuru anaonekana akipinda uso wake na macho kama jinsi watoto wafanyavyo wapowachezea wenzao.

Uhuru aliamua kuleta ucheshi wakati ambapo alikuwa akitambuliwa na mwanadada mmoja kwenye hafla moja.

Habari Nyingine: Mashemeji derby: Kipkurui aizamisha AFC Leopards

Hijabainika ni vipi rais aliamua kurejelea mchezo huo wa utotoni ambao huwa maarufu sana haswa kwa watoto wa kike.

Hata hivyo, sekunde hizo chache za rais ziliwasha moto kwenye mitandao huku wanajamii wakiendeleza ucheshi kwa kutengeneza ‘memes’.

READ ENGLISH VERSION

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected]; [email protected] au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending