– Uzinduzi rasmi wa Bandari Kavu ya Kontena mjini Naivasha itakayopokea shehena kutoka Mombasa kutumia Reli ya Kisasa SGR ulifanywa na Rais Uhuru Kenyatta
– Kuzinduliwa kwa huduma hiyo kunatarajiwa kuboresha maendeleo katika eneo la Afrika Mashariki ikiwemo Burundi, Rwanda, Uganda, Sudan Kusini na maeneo ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC)
– Reli hiyo ina leni nne za kusafirishia abiria kutoka vituo vya; Ongata Rongai, Ngong, Mai Mahiu na Suswa na kituo kimoja cha kubadilishia leni kilichopo eneo la Nachu
– Mjumbe maalum wa Rais wa Uchina Wang Yong ni miongoni mwa wageni wawakilishi wa washirika katika mradi huu waliohudhuria
Rais Uhuru Kenyatta Jumanne, Disemba 17, alizindua rasmi Bandari Kavu ya Kontena mjini Naivasha itakayopokea shehena kutoka Mombasa kutumia Reli ya Kisasa SGR.
Bandari hiyo kavu (ICD) ipo kwenye reli mpya ya Nairobi-Suswa ambayo iliigharimu serikali KSh 150 bilioni. Inapita miji ya kaunti za Nairobi, Kajiado, Narok na Nakuru.
Rais Uhuru Kenyatta wakati wa uzinduzi rasmi kituo cha Reli ya Kisasa SGR cha kusafirisha shehena kutoka Nairobi hadi depo ya Kontena mjini Naivasha. Picha: PSCU Source: UGC
Reli hiyo ina leni nne za kusafirishia abiria kutoka vituo vya; Ongata Rongai, Ngong, Mai Mahiu na Suswa na kituo kimoja cha kubadilishia leni kilichopo eneo la Nachu.
Kuanza kwa oparesheni za reli hiyo ya SGR kunatarajiwa kuboresha maendeleo katika eneo la Afrika Mashariki ikiwemo Burundi, Rwanda, Uganda, Sudan Kusini na maeneo ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC).
Kwenye hafla hiyo inayofanyika huko Syokimau, mjumbe maalum wa Rais wa Uchina Wang Yong ni miongoni mwa wageni wakilishi wa washirika katika mradi huu. Picha: The Standard Source: UGC
Rais Uhuru alisema kuwa, serikali yake imejitolea kuboresha miundombinu kote nchini ili kuifanya Kenya kuwa kituo cha wawekezaji.
Alisema kazi ya kuboresha na kuanzisha huduma za reli ya zamani eneo la 2B kwenda Malaba inaendelea.
“Huduma ya kusafirisha kwenda Naivasha itasaidia sana katika kuondoa msongamano Nairobi na Mombasa na pia kurahisisha usafirishaji wa cargo kwenda maeneo ya Magharibi mwa nchi. Pia itasaidia Sudan Kusini, Rwanda, DRC na Uganda kupunguza muda wa kusafirisha shehena kutoka Bandari ya Mombasa,” alisema.
Kwenye hafla hiyo inayofanyika huko Syokimau, mjumbe maalum wa Rais wa Uchina Wang Yong ni miongoni mwa wageni wakilishi wa washirika katika mradi huu.