Connect with us

General News

Seneta Omanga amwonyesha Betty Kyalo jinsi ya kukata kiuno kwenye ‘dance floor’ ▷ Kenya News

Published

on


Seneta mteule Millicent Omanga amewasisimua mashabiki wake mtandaoni kwa ustadi wake katika kusakata densi kutumia mitindo ya kisasa.

Katika video ambayo imesambaa mitandaoni, Omanga anaonekana pamoja na mwanahabari Betty Kyalo akimfunza jinsi ya kukata kiuno.

Habari Nyingine: Kortini: Mzee Moi atakiwa kulipa KSh 1B kwa kunyakua shamba la ajuza

Mbinu ya kusakata densi ya Seneta Omanga yawasisimua mashabiki wake. Picha: UGC
Source: Instagram

Huku akiwa amejibeba kweli kweli, Seneta Omanga anaonyesha umahiri wake katika kunengua kiuno chake kinene licha ya umri wake.

Hatimaye Betty anabaki tu kuajabia na kujaribu mbinu ya Omanga ambaye anageresha mwili na kunengua chini kwa chini.

Habari Nyingine: Siwezi kumchumbia mwanamke asiyekunywa pombe

Seneta Omanga asisimua mtandao kwa kunengua kiuno mtindo wa kisasa

Seneta Omanga na Betty Kyalo wasisimua mtandao kwa kunengua viuno mtindo wa kisasa. Picha: Facebook
Source: Facebook

Wawili hao walikuwa nyumbani kwa Omanga ambapo mahojiano ya kipindi cha Up Close with Betty yalifanyika.

Mavazi ya wawili hao vile vile yaliwateka mashabiki wao.

Habari Nyingine: Hospitali ya Kijabe yasherehekea baada ya kumponya mtoto kutokana na ugonjwa wa saratani

Seneta Omanga asisimua mtandao kwa kunengua kiuno mtindo wa kisasa

Mwanahabari Betty Kyalo ambaye alikuwa akimhoji Seneta Omanga kabla ya wawili hao kuamua kukata viuno. Picha: UGC
Source: UGC

Mwanasiasa huyo mwenye umbo lenye mvuto kwa baadhi ya mashabiki wake alikuwa amevalia nguo nzuri na iliyombana vizuri mwilini huku Betty akitokea mzima mzima katika nguo yake ambayo pia ilikuwa imembana.

Subscribe to watch new videos

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke; obed.simiyu@tuko.co.ke au WhatsApp: 0732482690. Tufuate kwa Telegram: Tuko news.

Source: Tuko.co.ke

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending